HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2023

WANANCHI BUKOBA MJINI WAZIOMBA KAMPUNI ZA SIMU KUPELEKA HUDUMA YA MAWASILIANO YA SIMU NA 'INTERNET'

 


Na Mwandishi Wetu,Kagera

WANANCHI wa Kijiji cha Kyasha katika Kata ya Buhembe wilayani Bukoba Mjini wameziomba Kampuni za simu za Tigo, Airtel, Vodacom, Halotel, na TCCL kuwafikishia huduma za mawasiliano ya simu na huduma za internet yenye kasi kwa mitandao hiyo kwenye kijiji chao na kuunganishwa na dunia.

Wametoa maombi hayo kutokana na uwepo wa changamoto kubwa kwa muda mrefu sasa ya mtandao wa intanent , hivyo umefika wakati kwa kampuni hizo kujenga minara itakayosaidia kuleta huduma za mawasiliano (voice na data) kushika kwa haraka kwenye makazi yao.

Mkazi wa Kijiji cha Kyasha Nyangoma Baltazar amesema ipo haja ya kuwepo kwa mawasiliano sahihi wakati wote na sio kusuasua kama ilivyo sasa kwani mji huo una zaidi ya wakazi 1,500 na ni vema kufikishia huduma hizo kwa haraka Ili kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.

Kwa upande Wake Rwegasira Isaack ameeleza kuwa kampuni hizo zinatakiwa kuboresha huduma za kimtandao hususani katika maeneo ya Kyasha na maeneo mengineyo ya Kata ya Buhembe ambapo hali hiyo inasababisha Kampuni hizo kukosa mapato makubwa kwa wananchi ambao wapo tayari kuwa wateja wao na kuchangia pato la Taifa kwa njia ya kodi.

"Hali ya ukosefu wa intaneti kwetu imekuwa ni ya kawaida na kiukweli inatuathiri sana,tunafahamu kuwa Dunia ya Sasa ni ya utandawazi Kwa hiyo Ili tuweze kufikia lengo ni lazima kuwepo kwa mawasiliano yatakayo tuunganisha sisi watu wa Kyasha na sehemu nyingine duniani, kama hili litaweza kuchukuliwa hatua nzuri naimani ata Kyasha itaendelea kuwa na maendeleo makubwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao wa Kyasha wameiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kuwafikishia na kuwatatulia shida yao ya mawasiliano kama walivyotatuliwa shida ya maji hivi karibuni.

Ambapo wamempongeza na kumshukuru Rais kwa kuwaletea maji kijijini mwao na Kumtua mama ndoo kichwani na kuzidisha chachu ya maendelea kuzidi kukua.

Aidha wananchi hao wametoa rai kwa Makampuni ya simu kufikisha mawasiliano katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya vijijini Ili kusaidia kero hii kuisha na Hali ya mawasilimo kuwa shwari muda wote na kuwaunganisha Watanzania na dunia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad