HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 5, 2023

WANAKC SARANGA, WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWATEMBELEA WASICHANA WANAOLELEWA NA FAMILIA YA CONSOLA ELIYA

Picha ya Pamoja.
Baadhi ya WanaKC Saranga wakiwa katika Maandamano kuelekea kwenye familia ya Consola kwaajili ya kuwaona na kuwajulia hali wasichana wa wanaolelewa katika Nyumba hiyo.
Baadhi ya WanaKC Saranga wakiwa katika Maandamano kuelekea kwenye familia ya Consola kwaajili ya kuwaona na kuwajulia hali wasichana wa wanaolelewa katika Nyumba hiyo.
Diwani wa Kata ya Saranga Edward Laizer akizungumza na wanaKC Saranga Wakati wakiadhimisha siku ya Wanawake duniani ambayo hufanyika Kila Mwaka Machi 8, ambapo wanaKC walitembelea Familia ya Consola Elia na kutoa Mahitaji mbalimbali.

Mwenyekiti wa KC Saranga, Maria Mwigune akizungumza na Watoto wa Familia ya Consola Eliya pale walipotembelea na Kutoa vitu mbalimbali.
Mwenyekiti wa KC kata Kivule, Zahara Mzee akizungumza na watoto wa Familia ya Consola walipotembela wana KC Saranga kwaajili ya kuwapa Faraja na kutoa Elimu pamoja na kuwasaidia kazi mbalimbali katika Nyumba yao.

Diwani wa Kata ya Saranga Edward Laizer akimkabidhi vitu mbalimbali Dada Mkubwa wa Familia ya Consola, Nuru pale wanaKC Saranga walipotembelea Familia hiyo.
Dada Mkubwa wa Familia ya Consola, Nuru akitoa shukurani kwa niamba ya wasichana wanaoishi katika familia  hiyo walipotembelewa na Wanakituo cha Maarifa Saranga.

WAKITUO cha Taarifa na Maarifa Cha Saranga (Knowledge Centre, (KC) wa Kata ya Saranga Kimara Stop Over Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam washeherekea siku ya Wanawake duniani kwa Kutembelea Kituo cha New Hope for Girls cha Familia ya Consola Eliya iliyopo katika eneo hilo.

Familia ya Consola ni Familia ya Baba na Mama na Watoto wakike 58 wenye Mahitaji Maalumu ambao anaishi nao katika nyumba hiyo ikiwa ni katika kusaidia Wasichana ambao walitelekezwa, Waliokotwa na waliokuwa hawana mahalali pa kuishi ili na wao wakae katika Familia yenye Misingi ya Kumjua Mungu na Upendo.

Diwani wa Kata ya Saranga, Edward Laizer akizungumza wakati Walipofika katika Familia hiyo Machi 4, 2023 amewapongeza kwa kupata kibali cha kuishi katika familia ya Consola na kutimiza Ndoto zenu kama watoto wengine.

Laizer amewaasa kuachana na vitendo viovu na Vya Kikatili ambavyo vitaweza kuwarudisha kule walipokuwa mwanzo bila kutimiza malengo yao katika Maisha yao.

Akiwaasa Wana KC Saranga amesema kuwa wapaze sauti ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia unaofanywa na baadhi ya wanawake pamoja na familia fulani ili kila Mtoto aweze kulelewa kwenye Familia yenye maadili mema na kumpenda Mungu.

"Niwaase wana KC Saranga Muache kupigishana Shoti kwa maendele ya Kikundi chenu na kwa Maendeleo ya taifa na Kizazi kijacho."

Pia amewaomba wana KC Saranga wasione aibu kuwasemea watoto wenye mahitaji maalumu ili na wao wawe na watu wa kuwasemea pale zinapojitokeza changamoto mbalimbali.

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa KC Kivule, Zahara Mzee amewaasa wasichana wa Familia ya Consola kutumia vizuri Mitandao ya Kijamii kwani kilakitu kilichopo mitandaoni kinaishi.

Amewaomba kutumia mitandao hiyo kupata faida mbalimbali hasa kujisomea, kutafuta maarifa yanayohitajika pamoja na kujua namna ya kutafuta masoko ili kujiingizia kipato.

Mwenyekiti wa KC Saranga, Maria Mwigune amesema kuwa KC Saranga wameona umhimu wa kutembelea kituo hicho kwani kipo Karibu nao hasa ukizingatia Msemo wa 'huduma ianzie Nyumbani.'

Pia amewaomba wana KC Saranga kutokuishia hapo licha ya Kutoa matoleo mbalimbali ili kila mtoto aonje upendo wa wazazi au walezi wao.

Licha ya hayo Wana KC Saranga wamejitolea kutoa taka zote zitakazozaliwa katika familia ya Consola bila gharama yeyote.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Familia hiyo ambaye ni Dada Mkubwa wa Familia hiyo, Dada Nuru amewashukuru WanaKC Saranga na Diwani wa Kata ya Saranga kwa kuwatembelea na kuwapa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ushauri wa Kimawazo na Kiroho.

NB; Familia ya Consola Eliya Waliwahi kushinda tuzo ya Malkia wa Nguvu mwaka 2021, tuzo zilizokuwa zikitolewa katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere baada ya kuonekana kutunza wasichana zaidi ya 50 wenye mahitaji Maalumu kwa kuwalea kama watoto wake katika Familia yake.

Siku ya Wanawake duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8. Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu kuleta Usawa na Kijinsia."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad