HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 11, 2023

Wafanyakazi wa TCAA watakiwa kutumia muda wao wa kazi kuleta matokeo chanya kwenye Taasisi

 

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wametakiwa kuhakikisha wanatumia muda wa kazi kuiletea Taasisi yao manufaa badala ya kutumia muda huo kufanya mambo yasiyo na tija kwa muajiri.

Hayo yameelezwa leo Machi 11, 2023  na Meneja Rasilimali Watu na Utawala  Amina Silanda Ally wakati akifungua kikao kazi cha Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu  na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) 

"Tunatambua umuhimu wa chama cha Wafanyakazi katika kuchagiza mafanikio ya mamlaka, rasilimali watu ni muhimu kwa maendeleo ya taasisi kwahiyo TUGHE ina wajibu wa kuhakikisha inazungumza vyema na watumishi wanaotoka nje ya mstari,"amesema Amina

Kiongozi huyo amewasisitiza Wafanyakazi kutumia muda wao wa kazi kwenye uzalishaji badala ya kutumia rasilimali za umma kwa maslahi yao, huku akikemea tabia ya baadhi ya watumishi wanaoangalia tamthilia na kukaa kwenye mitandao ya kijamii maofisini badala ya kufanya kazi.

Amesema vikao hivi ni muhimu kwa kuwa vinaleta mshikamano na umoja kwa wafanyakazi ikiwemo kujadili changamoto wanazozipata wafanyakazi na kuzitafutia ufumbuzi kwani wao ni kama daraja kati ya utawala na wafanyakazi.

Mbali na hayo, Amina aliwataka watumishi wa TCAA kuwasilisha changamoto wanazokumbana nazo kwa mamlaka husika badala ya kusubiri vikao vya TUGHE kueleza changamoto wanazopitia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la TCAA Jackline Ngoda, amesema lengo la kufanya kikao hicho ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao katika utendaji ikiwa na kauli mbiu isemayo kuchaguza wafanyakazi wa usafiri wa Anga kufanya kazi kwa ufanisi na juhudi kwani hilo ndilo lengo la kuweza kuipaisha mamlaka hiyo.
Mgeni rasmi  Meneja Rasilimali Watu na Utawala  Amina Silanda Ally akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na viongozi wa TCAA pamoja na kumkaribisha Mgeni rasmi  Meneja Rasilimali Watu na Utawala  Amina Silanda Ally  kwa ajili ya kufanya ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mwakilishi wa Katibu TUGHE mkoa Dar es Salaam Anthelmus Tarimo akitoa mada kuhusu umuhimu wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi pamoja na namna chama hicho kinachoweza kumlinda mfanyakazi hasa anapotaka kufukuzwa kazi au akiwa anefukuzwa kazi wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa wawasilishwaji wa mada wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mgeni rasmi  Meneja Rasilimali Watu na Utawala  Amina Silanda Ally  akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad