HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 28, 2023

WAFANYAKAZI MZUMBE NDAKI YA DAR ES SALAAM WANOLEWA, WAASWA KUJIKITA, KUTAFUTA, KUTEKELEZA MIRADI

WAFANYAKAZI wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es salaam wapewa mafunzo juu ya huduma kwa Jamii jijini Dar es Salaam leo Machi 27, 2023 pia wameombwa kujikita katika kutafuta au kuomba ufadhili wa miradi mbalimbali ya utafiti ili kuweza kutekeleza mipango ya muda mrefu ya huduma kwa jamii. 

Akizungumza wakati akiwasilisha mada chuoni hapo Mwezeshaji ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Elgidius Ichumbaki amesema kuwa hilo linawezekana kwa kuhakikisha miradi mbalimbali ya utafiti inayotekelezwa inakuwa katika mrengo wa huduma kwa jamii. 

Amesema kuwa mjadala ulijikita katika kuelezana ni kwa namna gani huduma za jamii Chuo Kikuu Mzumbe zinaweza kuboreshwa.

Awali Mratibu wa Huduma za Jamii Dkt. Issaya Lupogo pamoja na Mudiri wa Idara ya Ushauri wa Kitaaluma na kozi fupi Dkt. Chamwali Lihoya waliwakumbusha kuwa kuna haja ya kusoma Sera ya Huduma kwa Jamii kwa sababu ilishapitishwa na Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe. 

Pia, waliwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kuwa Chuo Kikuu Mzumbe hutenga bajeti kwa kila kitengo ikiwemo Ndaki ya Dar es salaam kwa ajili ya kuduma kwa jamii na wamewasisitiza wafanyakazi kushiriki katika kutoka huduma kwa jamii hususani jamii zinazoizunguka Chuo Kikuu Mzumbe. 

Pamoja na mambo mengine waliyoshirikishana katika mafunzo hayo, ilibainika kwamba Chuo Kikuu Mzumbe kinatakiwa kuwekeza katika miradi ya muda mrefu ya huduma kwa Jamii badala ya kuwa na huduma kwa Jamii za muda mfupi.

“Hii itahusisha Chuo Kikuu Mzumbe kutoa huduma kwa jamii na kuwasimamia pamoja na kushirikiana nao hadi maarifa waliyowapa wanajamii yazae matunda ya kuwanufaisha au hadi matokeo chanya yaonekane kujitokeza.” Ameeleza Dkt. Lupogo

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es salaam, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Joshua Mwakujonga amesema kuwa warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo unaosisitiza kuwepo kwa warsha hiyo kila mwaka mara moja. 

Akizungumza katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Huduma za Umma (DPS) kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, amesema malengo ya Warsha hiyo ni kukumbushana na kufundishana kuhusu huduma za jamii ikiwemo kujuzana kuhusu sera ya huduma kwa jamii Chuo Kikuu Mzumbe iliyopitishwa na Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe mwaka 2022. 

Vilevile, ni sehemu ya kutekeleza kaulimbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe: TUJIFUNZE KWA MAENDELEO YA WATU. 

Akisisitiza umuhimu wa Warsha hiyo amewaomba washiriki kuzingatia maarifa waliyoyapata.

Aidha, Marehemu Prof. Prosper Ngowi aliyewahi kuwa Rasi wa Ndaki ya Dar es salaam alitajwa kuwa kati ya watu ambao walikuwa wakishiriki katika kutoa huduma kwa jamii kwa kiwango kikubwa, hivyo walikumbushana kumuenzi kwa kufuata nyayo zake katika hilo.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na wanatalaamu na wafanyakazi waendeshaji huku kukiwa na mjadala shirikishi unaovutia ikiambatana na baadhi ya wafanyakazi akiwemo Dkt. Faisal Issa kutoa uzoefu wao wa kutoa huduma kwa jamii na ikafungwa na Dkt. Kanty Mtey kwa kuwashukuru washiriki na  kuwahimiza washiriki kuhakikisha wanaiishi elimu waliyoipata.
Mratibu wa Huduma za Jamii Dkt. Issaya Lupogo akizungumza na Wafanyakazi  wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es salaam wakati wa mafunzo yaliyofanyika Machi 27, 2023.
Mwezeshaji ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Elgidius Ichumbaki  akizungumza na Wafanyakazi  wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es salaam wakati wa mafunzo yaliyofanyika Machi 27, 2023.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Kanty Mtey akiwashukuru washiriki wa mafunzo Machi 27, 2023.

Wafanyakazi  wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es salaam wakisikiliza mada.

Wafanyakazi  wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es salaam wakiwa katika Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad