TMDA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO KULINDA AFYA YA MTUMIAJI HUDUMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 10, 2023

TMDA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO KULINDA AFYA YA MTUMIAJI HUDUMA

  Na Dennis Gondwe, DODOMA
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya kati imetoa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa na vifaa tiba waliokasimiwa majukumu hayo ili kuwajengea uwezo wa kukagua ubora wa bidhaa hizo katika soko na kumhakikishia huduma bora mtumiaji.

Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya kati Dodoma, Sonia Mkumbwa alipokuwa akielezea umuhimu wa mafunzo hayo kwa kwa wakaguzi wa dawa na vifaa tiba yaliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Majengo Tanzania jijini Dodoma.

Meneja Mkumbwa alisema kuwa majukumu waliyowakasimisha ni ukaguzi, kufuatilia usalama wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi. “Kufuatilia na kutupa taarifa kama kutatokea madhara kwa jamii wanayoihudumia ili Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kwa mamlaka iliyonayo iweze kuchukua hatua stahiki. Jukumu lingine ni kufuatilia ubora wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika soko ambalo wao wakaguzi wametoka” alisema Mkumbwa.

Alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kwenda kutatua changamoto katika maeneo ya kutolea huduma. “Sehemu za kutolea huduma kuna bidhaa zenye ubora tofauti. Mfano bidhaa bandia na bidhaa duni. Kuna bidhaa nyingine tarehe ya kutumika bado ipo vizuri lakini kutokana na uhifadhi wake kuwa duni hakuna feni au kiyoyozi jambo linalosababisha kiwango cha ubora katika bidhaa ile kushuka” alisema Mkumbwa.

Mafunzo kwa Halmashauri 29 za Mkoa wa Dodoma yaliandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya kati kuwajengea uwezo wakaguzi wa dawa, vifaa tib ana vitendanishi ili waweze kulinda afya ya mtumiaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad