Katika kusherehekea sikukuu ya mwanamke duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu.
Tanzania Commercial Bank (TCB)
imetumia sikukuu hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake
wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocen Road na kutoa misaada
mbalimbali.
Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja
mawasiliano na uhusiano wa Benki hiyo Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa
"Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa
misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".
Ameeleza kuwa " Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo"
Aliwahamasisha
wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa
tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.
mutta aliongeza
kuwa benki ya TCB inatoa huduma nchi nzima ina matawi ambayo yanafanya
kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma
muda wowote.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Ocean Road
Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema
kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii
inayotuzunguka hususani sekta ya afya.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzanian Commercial bank (TCB), Gloria Mutta (watatu kulia) akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa Afisa Ustawi wa jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga Kwaajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam Ukiwa ni kusherehekea siku kuu ya wanawake inayofanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka wengine pichani ni wafanyakazi ya hospital hiyo Hafla hiyo imefanyika jana.
No comments:
Post a Comment