HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 26, 2023

TAA WAONGEZA WIGO, NDEGE YA SAUDI ARABIA YAZINDUA SAFARI ZAKE HAPA NCHINI


Baadhi ya abiria wakipanda ndege ya Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023 wakielekea Saudia. 
Ndege ya Shirika la Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) ikiwa katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam bara baada ya kutua leo Machi 26, 2023.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) leo Machi 26, 2023 wamepokea ndege ya Shirika la Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) yenye uwezo wa kubeba abiria 180 kwa wakati mmoja.

Shirika hilo, linafanya safari za kimataifa za ratiba maalumu katika nchi zaidi ya 100 duniani katika Mabara ya Afrika, Asia, Ulaya na Amerika Kaskazini. Katika bara la Afrika, Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi 14 ambazo shirika hili linakuwa na safari za moja kwa moja ambapo kwa kuanzia litafanya safari za JNIA kwenda Jeddah katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha King Abdulaziz.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (MB.) amesema kuwa ndege hiyo aina ya Aibus 320 itafanya safari zake kutoka hapa nchi kwenda nchini Saudia mara nne kwa wiki na itarahisisha usafiri kwa watanzania na abiria kutoka Tanzania kwenda moja kwa moja nchini Saudi Arabia.

Pia itawarahisishia wasafiri wa nchi jirani kuchagua njia ya usafiri wa moja kwa moja ambao ni nafuu na wa muda mfupi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu wanaokwenda kufanya ibada ya Hijja.

“Leo hii tunashuhudia moja ya matunda ya ziara ya Mheshimiwa Rais aliyofanya nchini Saudi Arabia mnamo Mwezi, Juni 2022. Ziara hiyo imewezesha kuongezeka kwa mashirika makubwa ya ndege ya Kimataifa yanayofanya safari zake nchini ikiwemo shirika hili la ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia.” Amesema Prof. Mbarawa

Ameongeza kuwa Maamuzi ya Shirika hili ya kuanzisha safari za ndege za ratiba maalum hapa nchini yamechagizwa kwa kiasi kikubwa pia na kuimarika kwa mazingira ya kibiashara na uwekezaji yaliyopelekea uhitaji wa usafiri wa anga wa moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Saudi Arabia

“Kabla ya kuanzishwa kwa safari za ndege za shirika hili, abiria walilazimika kupitia mataifa mengine ili kufika nchini Saudi Arabia ambapo uzoefu unaonyesha walitumia masaa takribani kumi (10) ili kukamilisha safari zao. Hivyo, kwa kutumia Shirika hili, abiria wataweza kusafiri kwenda Jeddah moja kwa moja na watatumia masaa takribani manne na dakika arobaini.” Ameeleza Prof. Mbarawa

Kwa Upande wa Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Fardi Al Harbi, amesema ujio wa ndege hiyo kutoka Saudi Arabia kutaongeza shughuli za usafiri wa anga, biashara na utalii kati ya nchi hizi mbili.

“Hii itangangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha na kuendeleza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.”

Amesema kuwa Ujio wa Ndege hiyo hapa nchini utasaidia katika biashara pamoja na mahujaji pamoja na watalii kutembelea maeneo ya utalii katika nchi zote mbili.

Akizungumzia ujio wa ndege hiyo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Mussa Mbura amesema ujio wa ndege hiyo ni matokeo ya maelekezo ya kuongeza mashirika ya ndege hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) za mwaka 2022, idadi ya abiria wa kimataifa nchini inaonekana kuongezeka kwa asilimia 55 kutoka abiria 1,694,085 katika mwaka 2021 hadi kufikia abiria 2,618,119 mwaka 2022.

Picha za pamoja.

Viongozi mbalimbali wakipata zawadi mara baada ya kuwasili Ndege ya Shirika la Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (MB.) akizungumza wakati wa mapokezi ya Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.
Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Fardi Al Harbi, akizungumza wakati wa mapokezi ya Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Jabir Mwadini akizungumza wakati wa mapokezi ya Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Mussa Mbura akizungumza wakati wa mapokezi ya Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (MB.) akisalimiana na baadhi ya wageni waliokuja na Ndege la Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (MB.) akishirikiana na viongozi mbalimbali kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege ya Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023.Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya abiria wakipanda ndege ya Serikali ya Ufalme ya Saudi Arabia (The Royal Kingdom of Saudi Arabia) katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2023 wakielekea Saudia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad