HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 14, 2023

SERIKALI HAIKUFANYA KOSA KUWEKA SOKO LA MADINI MIRERANI - MONEY


Na Mwandishi wetu, Mirerani

MWENYEKITI wa Kamati ya Taifa ya madini ya Tanzanite, Money Yusuf amesema She erikali haikufanya makosa kwa uamuzi wake wa madini ya Tanzanite ambayo hayajasanifiwa {rafu} kuuzwa katika Mji wa Mirerani kwani ilizingatia vitu vingi vya msingi hadi kufikia hatua hiyo.

Money ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) akizungumza na waandishi wa habari mji mdogo wa Mirerani amesema wanaolazimisha madini ya Tanzanite rafu yauzwe nje ya Mirerani hawana hoja za msingi kwani wanachukulia uamuzi huo kisiasa.

Amesema kwa sasa Serikali imeruhusu madini ya Tanzanite yaliyosanifiwa ambayo yameongezewa thamani kuuzwa nje ya Mirerani hususani katika maeneo ya vivutio vya kitalii,hotel kubwa za kitalii na maeneo mengine maalumu na kusema kuwa hilo wao haliwatii shaka kwani ndio biashara yenyewe na serikali imelidhia kwa mpangilio maalumu lengo ni kila mmoja kulipa kodi stahiki.

Mwenyekiti huyo amesema kwa sasa serikali ipoo katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha jengo la kufanyia biashara ya madini ya Tanzanite litakalojulikana kwa jina la ‘’Tanzanite City’’ lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 hivyo wafanyabiashara wote wa madini hayo tunapaswa kuiunga mkono serikali kwa jitihada hizo za kukuza biashara hiyo na mji mdogo wa Mirerani kwa ujumla

Akizungumzia jiwe la Tanzanite lililonunuliwa na serikali kutoka kwa Bilionea Saninu Laizer ambalo baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya ukubwa wa jiwe hilo na thamani ya fedha aliyopewa,Money alisema kuwa thamani ya jiwe haliangaliwi kwa ukubwa bali linaangaliwa kwa ubora na rangi yake na siyo vinginevyo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa jiwe la Tanzanite linaangaliwa katika vitu vingi ili liwe na thamani kubwa ikiwemo ubora wa jiwe unaokwenda sambamba na rangi yenye ubora wa hali ya juu unaokubalika katika soko la kimataifa na ndio thamani yake inakuwa kubwa na siyo kuangalia ukubwa wa jiwe bila kuzingatia vitu hivyo vinavyohitajika sokoni.

‘’Serikali ilinunua jiwe la Tanzanite kwa Bilionea Laizer kwa thamani ya jiwe na siyo ukubwa wa jiwe na fedha aliyoipata iliendana na ubora wake na siyo ukubwa,’’ amesema Money.

Amesema uamuzi uliotolewa na serikali juu ya soko la madini liwe katika mji mdogo wa Mirerani haukufanywa kwa kukurupuka bali ulizingatia mambo mengi ya msingi kwa maslahi ya nchi na wanataka soko hilo liwe jijini Arusha wana yao ila muda ukifika ataweka hadharani kwani wana maslahi yao binafsi na siyo ya nchi.

"Tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa amini wafanyabiashara wa Tanzanite na kusogezea huduma ya soko katika mji mdogo wa Mirerani na amemuomba kuwafikiria juu ya suala la zana za uchimbaji kupunguziwa kodi ama kuondoa kwani kwa sasa zipo kwa gharama kubwa na upatikanaji wake ni wa shida.

Amewataka wafanyabiashara wa Tanzanite kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada zake za kuhakikisha biashara hiyo inafanyika mji mdogo wa Mirerani ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki na kuwapuuza wale wote wanaotaka biashara hiyo kufanyika jijii Arusha.Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya madini ya Tanzanite na Makamu Mwenyekiti wa MAREMA, Money Yusuf akizungumza na waandishi wa habari mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad