HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2023

RAIS SAMIA ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA AFRIKA KUSINI NA MWENYEJI WAKE RAIS CYRIL RAMAPHOSA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Juu Kabisa ya Heshima inayotolewa na Rais wa Afrika Kusini. Tuzo hiyo amepewa na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa katika hafla fupi iliyofanyika mjini Pretoria Machi 16, 2023. 

Maelezo yaliyosomwa kuhusiana na Tuzo hiyo yamefafanua kuwa sababu za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutunukiwa tuzo hiyo ya Juu Kabisa ya Afrika Kuisni (The Order of South Africa) ni kumpongeza kwa kuandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia ameendelea kudumisha udugu wa kihistoria wa mataifa hayo mawili, Afrika Kusini inatambua mchango wa Kijeshi, Kijamii na Vifaa, kwa Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini uliotolewa na Tanzania wakati wa siku za kiza za ukandamizaji huko Afrika Kusini, ambapo kuanzia miaka ya mwanzo ya 1960 hadi Afrika Kusini ilipopata Uhuru, Tanzania ilikuwa nyumbani kwa wapigania Uhuru wa Afrika Kusini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivishwa nishani ya Juu kabisa ya Afrika Kusini (The Order of South Africa) na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa Machi 16, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati akizungumza na Wanahabari wakati wa Ziara yake ya Kiserikali Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati akizungumza na Wanahabari wakati wa Ziara yake ya Kiserikali Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati wakishuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi mbili, Pretoria nchini Afrika Kusini Machi16, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ziara yake ya Kiserikali, Pretoria nchini Afrika Kusini Machi 16, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mapokezi ya Viongozi vilivyopo kwenye Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuanza mazungumzo Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa yaliyofanyika katika Ofisi za Majengo ya Muungano, Pretoria nchini Afrika Kusini Machi 16, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad