*Usahili kufanyika Machi 12
Na.Khadija Seif, Michuziblog
SHINDANO la Miss Dar es Salaam Zone la zinduliwa rasmi huku Usahili unatarajiwa kufanyika Machi 12 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam Mratibu wa shindano hilo, Linda Samson ambaye pia alikuwa Miss Ilala mwaka 2018, amesema fainali ya shindano hilo litafanyika Mei mwaka huu huku akiwaomba warembo kujitokeza kwa wingi kwenye Shindano hilo.
"Lengo la shindano hilo ni kusaidia mabinti kufikia ndoto zao kupitia urembo pia Kuwajengea uwezo warembo kusaidia jamii zinazowazunguka
Ameongeza kuwa warembo kutoka wilaya ya Ilala, Temeke, Ubungo na Kigamboni ndiyo watafanyiwa usaili kasoro Kinondoni kutokana na kuwepo na mratibu wa shindano hilo kwa ngazi ya wilaya ya Kinondoni .
"Warembo wataingia kambini Mei Mosi mwaka huu, pia baada ya usaili watafanya kazi za kijamii kama kutembelea hospitali na kufanya usafi kwa sababu kipindi hiki utakuwa wakati was mfungo wa Ramadhani, " alisema.
Pia amezitaja sifa za mshiriki anatakiwa awe na umri kuanzia 18 hadi 23 awe ajaolewa wala kuwa na mtoto.
Aidha ametoa pongezi kwa wadhamini mbalimbali waliojitokeza kudhamini shindano hilo wakiwemo Kinywaji cha 7 hills,Miles Away pamoja na wengine mbalimbali.
Kwa upande wake Miss Ilala 2022 Beatrice Alex amesema Mashindano ya Ulimbwende yamekuwa yakisaidia wasichana wengine kufikia ndoto zao hivyo kuna haja kubwa kwa wadau mbalimbali kuhakikisha wanaunga Mkono na kushirikiana na waandaaji ili kila mwaka yawepo Mashindano hayo.
Hata hivyo ametoa ahadi ya kuwakaribu na Warembo watakaopatikana katika Mchujo na kuhakikisha watakaokwenda Kambini watakuwa warembo watakaoiwakilisha vizuri Miss Dar zone na kufikia Mashindano ya Miss Tanzania.
Mratibu wa Shindano la Miss Dar zone Linda Samson Akizungumza na Wanahabari Leo Machi 04,2023 mara baada ya Kuzindua rasmi shindano hilo linalotarajiwa kufanya usahili wake mapema machi 12,2023 Jijini Dar es salaam akiwaalika wadau mbalimbali kudhamini shindano hilo pamoja na warembo kujitokeza kwa wingi
Meneja wa Kampuni ya Miles Away Ibrahim Mkulul Akizungumza namna Kampuni hiyo ambayo wamejitoa kudhamini Shindano la Miss Dar zone itahakikisha Warembo wanafanya utalii ndani na nje ya nchi
Miss Tanzania Mshindi wa 3 Beatrice Alex akizungumza na Wanahabari Leo Machi 04,2023 namna Kamati hiyo ilivyojipanga kuanzia usahili hadi Kambini kuhakikisha Warembo bora wanapatikana
No comments:
Post a Comment