HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 30, 2023

KIWANDA CHA BOSPHORUS MANUFACTURING CHAJA NA KIBOKO YA FANGASI ZA UKUTA IJULIKANAYO KWA JINA LA 'YAPFIX WALL PUTTY'.

 Uongozi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing kinachojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za kujengea kimetoa mwito kwa Watanzania kutumia bidhaa za kampuni hiyo ili kuzifanya nyumba zao ziwe imara na zidumu kwa muda mrefu zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 30,2023 jijini Dar es salaam,Meneja masoko wa kiwanda hicho Alex Kaaya amesema umefika wakati sasa kwa Watanzania kutumia bidhaa bora kutoka kampuni ya Bosphorus Manufacturing inayozalisha bidha ya Yapfix wall putty inayotumiwa kwenye kuta za nyumba wakati wa kupaka rangi.

Amesema kupitia Yapfix wallputty sasa watanzania hawatakuwa na hofu ya kuhofia kuta za nyumba zao kupata fangasi, kwani imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ambao utaifanya kuta za nyumba kutopata magonjwa wala bakteria.

'' Kwa kipindi hiki cha mvua katika maeneo mbalimbali nchini ni muhimu kwa watanzania kutumia bidhaa ya 'Antifangus Wallputty', ambayo haiingizi maji kwenye ukuta na kuifanya rangi kubanduka, hivyo nyumba itakaa muda mrefu sana baada ya kupakwa bidhaa hiyo'',amesema Kaaya.

Kaaya amefafanua kuwa kwa kutambua pia umuhimu wa kuweka vigae (tiles) katika nyumba wamekuja na gundi maalum ambayo hutumika kuwekea tiles katika nyumba bila kuichanganya na mchanga wala saruji na badala yake hutumia maji pekee katika uchanganyaji wake.

Amesema imefika wakati sasa kwa watanzania kufanya ulinganifu wa bidhaa za Wallputt kutoka kampuni hiyo na kampuni nyingine ili kugundua ubora wa bidhaa za kiwanda hicho ambacho kimewekeza zaidi ya bilioni 2 hapa nchini

"Napenda kuwaambia mafundi kuwa wakati wa kuchanganya saruji na mchanga katika kuweka tiles majumbani imepitwa na wakati kwani kwa sasa sisi kama kiwanda cha Bosphorus tumekuja na gundi maalum ya kuwekea tiles ambayo hutumia maji pekee katika uwekaji wake"alisisitiza Bw Kaaya.

Hata hivyo ameongeza kuwa kiwanda hicho hutumia teknologia ya kituruki katika uandaaji wa bidhaa zake jambo ambalo limeongeza ubora wa bidhaa

Kuhusu ajira katika kiwanda hicho amesema wameajiri zaidi ya watu 35 ambao hufanya shughuli za uzalishaji kiwandani hapo ambapo asilimia kubwa ya uzalishaji wa bidhaa hutegemea teknolojia huku malighafi za kutengeneza bidhaa za kiwanda hicho ikiwemo mawe na mchanga zikinunuliwa kutoka kwa wafanyabishara hapa hapa nchini.

Kwa upande wake Bw Ramadhan Hassan ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa za ujenzi katika eneo la Tabata amewaambia waandishi wa habari kuwa tangu aanze kuuza bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho zaidi ya miaka saba iliyopita mpaka leo amekuwa akipata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wake wakieleza ubora wa bidhaa za kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akieleza namna malighafi za mawe wanazotumia kuzalisha Gundi Yapfix mbayo ni maalum kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akieleza namna Gundi Yapfix mbayo ni maalum kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo yenye uwezo mkubwa wa kuzuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani,inavyofanya kazi kwa urahisi na haraka.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Alex Kaaya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar ers Salaam kuhusu Gundi maalum ya Yapfix inayotumika kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Necmetin Keles na Fundi Shabani Athuman (kushoto).

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akionyesha malighafi za mawe wanazotumia kuzalisha Gundi Yapfix mbayo ni maalum kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani, jijini Dar es Salaam.

Bidhaa hiyo ikiwa tayari kiwandani ikisubiri kupelekwa sokoni 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad