Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA
wamehamasishwa kuongeza nguvu katika matumizi ya nishati safi ya
kupikia ili kuondokana na athari mbalimbali zikiwamo za mazingira huku
matumizi ya nishati safi ya kupikia yakitajwa kuwa sehemu ya mkakati wa
kuendeleza uchumi kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho la
Kampuni za Gesi nchini Tanzania, Araman Benoite ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Oryx Gas nchini alipokuwa akizungumza kwenye Kongamano la Kampuni za
Gesi Afrika Mashariki linaloendelea jijini humo.
"Tutumie
fursa ya gesi ya kuwekeza ili kuwafikia wananchi wengi ambao bado
hawjaanza kutumia nishati safi ya kupikia. Pia tuitumie fursa hiyo
kuwekeza na kuimarisha uchumi," amesema Benoite.
Benoite
ameongeza kwamba bado kuna fursa ya uwepo wa soko kubwa la gesi ya
majumbani kwani Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
imejipambanua kuhamasisha matumizi yake.
Akizungumzia
umuhimu wa kufanyika kwa kongamano hilo amesema ni sehemu ya
kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ina faidi
mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Benoite, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kusaidia
mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira, kuunga mkono jitihada za
kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutumia muda mchache katika shughuli
za mapishi tofauti na pale endapo wangetumia nishati nyingine kupikia
kama Kuni au mkaa.
Akifafanua
kwa nini kongamano hilo limefanyika Tanzania, amesema ni moja ya
mkakati wa Kampuni za gesi kuunga mkono jitihada za Serikali
inayoongozwa na Rais Samia kufungua fursa za uwekezaji katika sekta ya
nishati ya gesi.
Kongamano
hilo limehudhuriwa na wadau kutoka nchi mbalimbali ikiwamo za Jumuiya
ya Afrika Mashariki zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na kampuni
za Kimataifa zinazokijusisha na biashara ya gesi duniani.
Awali
akisoma hotuba ya ufungui wa kongamano hilo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Mkurugenzi wa Shirikisho
hilo duniani Catherine Ho, alisema kongamano hilo litakuwa jukwaa muhimu
katika kuongeza uelewa na kukuza uwekezaji katika sekta ya nishati
hususan gesi ya majumbani (LPG) nchini Tanzania.
Amesema
zaidi ya washiriki 800 walisajiliwa katika kongamano hilo wakiwemo
wataalamu wa nishati ambapo pamoja na mambo mengine wataonyesha jinsi
sekta hiyo ilivyo muhimu katika kukuza uchumi.
Pamoja
na mambo mengine kwenye Kongamano hilo la Kimataifa,pia wameanzisha
Shirikisho ngazi ya Tanzania ambalo litakuwa likisimamia na kutoa
muongozo kuhusu masuala mbalimbali kwenye sekta ya nishati ya gesi.Mwenyekiti
wa Shirikisho la Kampuni za gesi Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Oryx Gas Araman Benoite akitoa hotuba kwa niaba ya kampuni
hizo leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Shirikisho hilo
Afrika Mashariki ambalo litafanyika kwa siku mbili nchini Tanzania
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Kampuni za gesi Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Oryx Gas Araman Benoite akijadiliana jambo na baadhi ya
wadau baada ya kumaliza kuzungumza katika Kongamano la Kimataifa la
Shirikisho la Kampuni za gesi Afrika Mashariki linaloendelea nchini
Tanzania
Wadau
wa Kampuni za Gesi Afrika Mashariki na mataifa mengine duniani wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kufunguliwa kwa Kongamano la Kimataifa
la Shirikisho la Kampuni za Gesi Afrika Mashariki ambalo litafanyika kwa
siku mbili katika Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania ambapo
washiriki 800 wameshiriki.
Matukio
mbalimbali katika picha wakati wa Kongamano la Kimataifa la Shirikisho
la Kampuni za gesi Afrika Mashariki likiendelea jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment