HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 27, 2023

IMO yatoa mafunzo kwa wakufunzi wa Ubaharia

  *Mafunzo hayo ni kwendana na viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma za ubaharia


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KATIKA kukabiliana na changamoto ya upungufu wa mabaharia nchini Shirika la Bahari Duniani IMO limetoa Mafunzo kwa Wakufunzi wa Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) Watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA).

Akizungumza wakati wa Kufuga wa mafunzo ya viwango vya walimu wa mabaharia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Wakili Rajab Moses amesema kuwa kila mwaka katika Chuo cha DMI wanafunzi wanaohitimu idadi yao ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo hivyo lengo DMI ni kutengeneza walimu wa kuwafundisha mabaharia na maafisa melini ili kiendana na viwango vya kimataifa vilivyowekwa.

Tanzania kwa sasa inakwenda katika uchumi wa Bluu hivyo kuwa na wataalam mabaharia ni jambo linafanya kuwa na uwezo wa uchumi mkubwa.

Wakili Moses amesema idadi ya wanaomaliza haikidhi Matakwa ya ya sekta ya ubaharia Duniani hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza idadi ya mabaharia nchini wenye kuendana na sifa za kimataifa.

Ametoa wito kwa mabaharia nchini kujiendeleza kitaaluma ilikuweza kupenya katika soko la Ajira lillopo nje ya nchi na ndani ya nchi.

"Kumekuwa na upungufu wa mabaharia hapa nchini na Duniani kwa ujumla,hii fursa ya kipekee kwa watanzania kujiunga na chuo cha DMI na wanafunzi wapatiwe ujuzi ambao ni bora na unaoendana na soko la kimataifa".Amesema Mkurugenzi Rajab.

Ameongeza kuwa kumekuwa idadi ndogo ya watalamu wazawa inayohatarisha ajira kupitia sekta hiyo jambo ambalo hufanya taasisi hiyo kuajiri mabaharia wa kigeni ila kupitia mafunzo hayo watapata wataalamu bora wenye ushindani kimataifa na wanakidhi vigezo.

"Mafunzo haya yamelenga wanafunzi wasio enda kwenye kozi ya ubaria ili kuongeza idadi ya watu wenye uzoefu na taaluma hiyo hapa nchini".Amesema Mkurugenzi wa Huduma za Shirika, Rajabu Moses

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo ya ubaharia Naho. Haruna Ally amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiajiri watu wenye ujuzi wa ubaharia.

Hata hivyo, amesema kuwa lengo ya mafunzo hayo ya siku tano nikuongeza mbinu na ujuzi pamoja na kuzalisha walimu wakuwafundisha wengine.

"Suala la ukosefu wa vifaa limekuwa ni kikwazo katika utoaji wa mafunzo hayo ya ubaharia. Changamoto hii kwetu imekuwa kubwa na inatuathiri.Amesema Mkufunzi Captain Haruna.
Mkufunzi wa Mafunzo ya Ubaharia Haruna Ally akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama kuhusiana na mafunzo hayo katika kuwezesha kuwa na viwango vya kimataifa vya ubaharia jijini Dar es Salaam.
Wakufunzi na Walimu wa Ubaharia wakiwa na Vyeti mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku tano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Wakufunzi na Mgeni Rasmi  Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa TASAC Wakili Rajab Moses mara baada ya kufunga mafunzo ya Siku Tano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Wakili Rajab Moses akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku Tano ya  Wakufunzi wa  Walimu wa Ubaharia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad