HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 24, 2023

Halotel yatoa Msaada wa vifaa vya Usafi Manispaa ya Mjini Zanzibar

 Kampuni ya Mawasiliano ya simu Halotel kupitia imekabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia Usafi kwa Manispaa ya Mjini Zanzibar, ikiwa ni moja ya msaada wa kuhakikisha Mji wa Zanzibar unatunzwa kwa usafi na kukuza shughuli za kitalii na uchumi wa mji huo ikiwa ni sambamba na kuadhimisha miaka miwili ya Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Dkt Hussein Ali Mwinyi.


Kampuni ya Halotel inayo sera ya kurejesha Kwa jamii.Sera hiyo imejikita katika kuhahakikisha kuwa wajibu wa kushirikiana na taasisi binafsi na za serikali katika kuboresha ustawi wa jamii, ilikuchochea maendeleo ya Taifa na watanzania kwa ujumla katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu.

Akizungumza wakati wa tukio la makabidhiano ya vifaa hivyo katika viwanja vya Malindi Zanzibar, Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Halopesa, Magesa Wandwi, alisema kampuni hiyo na sera ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii, taasisi binafsi na za serikali kuimarisha ustawi wa jamii.

“Tumeamua kutoa vifaa vya usafi na mabango ya elimu kwa wananchi juu ya wajibu wa ushirikiano katika kutunza mazingira na kuuweka mji katika hali nzuri kuvutia watalii na wenyeji. Hatua hii ni sehemu ya kampuni yateu na kuwaunga mkono kazi nzuri zinazofanywa na uongozi wa awamu ya nane chini ya Rais Dr. Mwinyi, ambae anaonekana kwa moyo wa dhati kutaka kuweka mji wa Zanzibar katika hali ya kupendeza na kuwa kivutio kikuu cha wageni wanaoingia hapa nchini,”alisema Magesa.

Aidha Magesa aliongeza kuwa “Nina matumaini kuwa vifaa hivyo vitatuzwa na vitawekwa katika sehemu zote zinazostahili kwa matumizi sahihi ili vitumike katika matumizi yaliyokusudiwa”.

Akipokea vifaa hivyo wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya Malindi Zanzibar Mkuu wa Wilaya ya Manispaa ya Mjini Mhe Rashid Simai Msaraka ameihakikishia kampuni ya Halotel kuwa Manispaa ya Mjini itatengeneza mkakati madhubuti wa usafi wa mji kupitia vifaa hivyo.

“Kwa muda mrefu Manispaa hii imekuwa ikitafuta mbinu ya kukabiliana na changamoto ya uchafu lakini kupitia msaada huu kutoka kampuni simu ya Halotel, umetufaa sana na baraza litahakikisha linawashughulikia wale wote wanaotupa taka hovyo katika maeneo mbalimbali ya mji.”

“Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza kampuni ya Halotel kwa kuliona hili na kutuunga mkono kwa kutuletea vifaa hivi muhimu, ninawaagiza watendaji wa manispaa hii kutimiza wajibu wenu ili mji uwe safi. Ninaiomba jamii pia kutambua kuwa suala la usafi si la manispaa pekee bali ni watu wote, hivyo baraza lina haki ya kumshughulikia kila atakayekwenda kinyume na utunzaji mazingira.” Alisisitiza Mh. Msaraka.

Zaidi ya shilingi Milioni 54 kutoka Kampuni ya Halotel zimetumika kwaajiliya kunua vifaa vya kusafishia mji ikiwemo 4 wheel Dustbin za lita 660, jumla 10, 2 wheel Dustbin za lita 240 zikiwa 50, mabwela suti 100, fagio 100, reki 100, toroli50, Shovel 50, glovu 100, bibs 100.

Halotel inaendelea kusambaza miundo mbinu ya Mawasiliano na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watanzania wote kama ilivyokuwa dhima ya serikali kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi katika maeneo yote.

Katika kuboresha huduma hii ya Mawasiliano Kwa wateja wetu, Kwa mwaka 2022 kampuni imeongeza minara mipya zaidi ya kumi na saba (17) ya masafa ya 4G ambayo ni kwa Upande wa Unguja na kwa kisiwa cha Pemba, inayowawezesha kupata huduma bora za intaneti.

Naibu Mkurugenzi wa Halopesa Magesa Wandwi (kulia katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mjini Iliyopo Zanzibar Mh. Rashid Simai Msaraka ( kushoto katikati) moja ya vifaa vya usafi kama ishara wakati wa tukio la makabidhiano ya vifaa vya Usafi vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 54 katika eneo la viwanja vya Malindi Zanzibar. Pamoja nao ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini (wa tatu kulia mbele) baadhi ya wafanyakazi wa Halotel na wawakulishi kutoka vikundi mbalimbali vya usafi wa Manispaa ya Mjini Zanzibar.
Vifaa vya usafi vilivyotolewa kwa Manispaa ya Mjini iliyoko Zanzibar kwaajili ya usafi.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad