HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 28, 2023

Wanawake waiomba serikali ipunguze gharama za matibabu ya saratani





Njombe
WANAWAKE wilayani Njombe wameiomba serikali isaidie kupunguza ghalama za matibabu ya kansa (saratani) ili kunusuru uhai wa wananchi wengi wenye kipato cha chini wanaofariki kwa ugonjwa huo kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Wito huo umetolewa na baadhi ya wanawake wilayani humo mara baada ya kamati tendaji ya Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) kutembelea wagonjwa pamoja na watu wenye mahitaji kata ya Lupembe na kuwafariji ambapo imetajwa kuwa tatizo la kansa limekuwa likiwatesa sana baadhi ya wagonjwa wilayani humo.

"Kwenye kata yetu ya Lupembe tuna wagonjwa wa kansa akiwemo mtoto,tunaiomba serikalina Rais Samia atusaidie kwenye matibabu ya watu wanaougua magonjwa ya kansa kwasababu sasa hivi tumeshampoteza mtoto mmoja na tuna mtoto mwingine ambaye bado anaumwa na hali ni ngumu"Alisema Faraja Mbanga diwani wa viti maalum kwa niaba ya wanawake

Naye mtendaji wa kijiji cha Lupembe Mery Ng'umbi ameshukukuru Jumuiya hiyo kutembelea katika kijiji chao na kuona makundi hayo ya watu ambapo amesema kuwa uongozi wa kata utaendelea kuwa karibu ili kuweka wazi changamoto zinazowakabili wananchi wao.

Miongoni mwa mgonjwa aliyetembelewa na jumuiya hiyo ni pamoja na Tulinave Matimbwi ambapo msimamizi wa mgonjwa huyo ameshukuru kwa kutembelewa na kupewa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo sabuni na sukari huku akibainisha kuwa msaada huo ni muhimu katika familia yao.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema jumuiya hiyo imechukua swala hilo kwa uzito na kwamba jukumu lao lililobaki ni kufikisha kwenye vyombo husika ili kuona namna ya kuisaidia jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad