Na Mwandishi wetu-TANESCO
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa mara ya kwanza limeanza kupokea moja ya mashine umba (Transforma) kubwa sita yenye uwezo wamegavoti 250 katika kituo cha kupokea na kupoza umeme mkubwa cha Chalinze ambapo kati ya mashine umba hizi sita,mashine umba nne zitakuwa zikipokea umeme mkubwa wa kilovoti 400 utakaosafirishwa kutoka katika Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) nakuupozahadikilovoti 220 na mashine umba mbili ni kwa ajili ya kuupoza umeme mkubwa kutoka kilovoti 220 hadikilovoti 132.
Akiongea mara baada ya kupokea mashine umba (Transforma) hiyo Chalinze mkoani Pwani ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, amesema kituo cha kupokea na kupoza umeme mkubwacha Chalinze kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 128 na mpaka sasa ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 53.13 na unatarajiwa kukamikiaifikapo tarehe 30 Julai 2023ambapo kituo kitaweza kusafirisha hadi megawati 800 za umeme katika miundombinu ya umeme iliyopo sasa hivi.
“Kituo hiki ambacho ndio kinapoza umeme kwa hapa Chalinze kitagharimu shilingibilioni 128 na ujenziwake umeshakamilika kwa asilimia 53.13.Leo tumepokea Transfoma kubwa kabisa, ni transfoma ya kwanza ambayo itafungwa hapa kimsingi kituo hiki kitafungwa transfoma sita na Reactors mbili na vifaa vyote vimeshafika katika bandari yetuya Dar Es Salaam.
Matarajio
yetu ni kwamba kituo hiki hadi kufikia Julai 2023 mwaka huu kitakuwa
kimeshaanza kusafirisha hadimegawati 800 za umeme kupitia miundombinu
ya umeme iliyopo, kwa hiyo haya ni mafanikio makubwa watanzania lazima
tujivunie kwa sababu umeme ni uchumi, umeme ni uhai, umeme ni maisha na
umeme ni maendeleo” amesema Mhe. Kunenge
Aidha
Mhe.Kunenge ameeleza kuwa mradi wa umeme wa bwawa la Julius Nyerere
utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika hasa kwa Mkoa wa Pwani ambao
utasaidia sana katika kuendeleza ukuaji wa viwanda katika mkoa huo.
“Mkoa
wa Pwani umeme kwetu ni jambo kubwa kama ilivyo kwenye maeneo mengine,
kwa hiyo kwa kituo hiki kufanya kazi maana yake ni kwamba Bwawa la
JuliusNyerere linazalisha umeme wa kilovoti 400 ambao utasafirishwa na
kupokelewa hapa na Transifoma hizi zitaupunguza mpaka kilovoti 220 na
trasforma nyingine mbili zitauunguza umeme kutoka kilovoti 220 hadi
kilovoti 132 ili uweze kutumika katika Gridiyetu na katika mfumo wetu
wa umeme maana yake ni kwamba inaleta ahueni kwanza kwa kupatikana
umeme mwingi na wa uhakika na wamiliki viwanda wanahitajiumeme wa
uhakika kwa hiyo nipende kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuuendeleza
Mradi huu wa Umeme” alishukuru Mhe. Kunenge.
Kwa
upande wake Meneja miradi waS hirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mhandisi Didas Lyamuya ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza na kujenga
viwanda vingi Mkoani Pwani kwa sababu kukamilika kwa kituo hiki cha
kupokea na kupoza umeme mkubwa cha Chalinze kitawezesha upatikanaji wa
umeme wa uhakika katika mkoa huo lakini pia mikoa ya jirani kama Tanga,
Arusha, Dodoma na Dar Es Salaam.
“Hiki
kituo kinapokea umeme ambao unatoka Julius Nyerere na kufanya umeme
wetu unaozalishwa Kinyerezi, Kihansi,Tegeta, Songasi na Ubungo kuja hapa
na kuanza kusafirishwa, kwa hiyo wakazi wa Mkoa wa Tanga, Arusha,Dodoma
na Dar Es Salaam watanufaika na kituo hiki kwa sababu nyaya zetu na
miundombinu yetu ilikuwa imetengana lakini sasa zote zitaanzia hapa, kwa
hiyo wananchi na wakazi wa hapa watakuwa na umeme wa kutosha kwa hiyo
ni wakati mzuri sasa kwa wawekezaji kuweka viwanda kwa sababu
tunauhakika na umeme wa kutosha” amesema Mhandisi Lyamuya.
Aidha,
kituo hiki cha kupokea na kupoza umeme mkubwa cha Chalinze chenye
thamani ya shilingi bilioni 128 zinazogharamiwa kwa asilimia 100 na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kilianza kujengwa mnamo
mwaka 2021 na mkandarasi TBEA kutoka China. Aidha, ujenzi wa kituo hiki
umefikia asilimia 53.13 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30
Julai, 2023.
No comments:
Post a Comment