MCHEZAJI wa Pool wa timu ya Taifa, Abdallah Hussein kutoka Klabu ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani, Dar es Salaam, ameteuliwa na Chama cha Pool Taifa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Duniayanayotarajiwa kufanyika nchini China, yajulikanayo kama“World Heyball Championships 2023”.
Uteuzi wa Hussein umekamilika leo Februari 16 baada yamchakato uliofanywa na viongozi wa chama hicho, akibebwauwezo mkubwa alioonyesha katika mashindano kadhaayaliyopita pamoja na kuwa na hati ya kusafiria (Passport).
Mwenyekiti wa Chama cha Pool, Isaac Togocho, amesema Hussein ataambatana na kiongozi mmoja wa chama hichoambaye atamteua hivi punde.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Machi 21 – 27,2023 kwa hatua ya awali ya kufuzu na Machi 28 ni sherehe zaufunguzi rasmi wa fainali zenyewe zitakazoanza siku inayofuatana kuhitimishwa Aprili 5,2023.
God bless young Dullah.
ReplyDelete