HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2023

Bilioni 3.1 za ruzuku zatolewa na LSF kuimarisha haki nchini

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal service (LSF) Lulu Kwakilala

SHIRIKA la Legal Services Facility (LSF), limetoa ruzuku ya kiasi Cha Sh. 3.1 bilioni kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji haki nchini hususan kwa wanawake na watoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng'wanakilala,ameyasema hayo leo tarehe 23 Februari 2023,na fedha hizo zimetolewa kwa wadau ikiwemo katika mashirika wanachama wanaotoa msaada wa kisheria, mashirika simamizi kwenye kanda sita na mashirka yanayotekeleza miradi kwenye maeneo muhinu ya kijamii hasa uchumi.

Amesema fedha hizo zimetolewa ili kuongeza ubora, uwezo na maendeleo ya kitaasisi katika kutoa huduma Bora za msaada aa kisheria kwa 2023, ambapo kiasi cha Sh. 2.08 bilioni kimepelekwa moja kwa moja katika mashirika 184 ya watoa huduma hizo Tanzania Bara na Zanzibar.

“Ruzuku inayotolewa kwa mashirika ya watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria inakwenda kuchochea pia utekelezaji mkakati wa kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia uliojikita kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto kwa kutoa elimu katika jamii kuhusu haki za biandamu, kupambana na ukatili wa kijinsia, utatuzi wa migogoro ya ardhi, masuala ya mirathi, kuelimisha wananchi kuhusu mifumo ya sheria, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala pamoja na kujenga uwezo miongoni mwa wadau wa sekta ya msaada ya kisheria nchini," amesema Ng'wanakilala.

Ametaja baadhi ya mashirika yaliyonufaika na ruzuku hizo, ikiwemo Shirika la Kilimanjaro Women Information Exchange and Community Organization (KWIECO), kwa ajili ya kutekeleza mradi kwenye eneo la utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala ya usukuhishi.

Sehemu nyingine ya ruzuku imetolewa na LSF kwa mashirika matatu kwa ajili ya kutekeleza miradi katika maeneo maalumu ya kiuchumi, kwenye sekta ya kilimo, madini, na uchumi wa bahari kwenye mikoa ya Manyara na Lindi, kupitia taasisi tatu za Community Support Initiatives Tanzania (COSITA), Lindi Association of Non-Governmental Organizations (LANGO), na Civic Social Protection Foundation (CSP).

Pia, LSF kwa kushirikiana na COSITA itawezesha wanawake kupata fursa zitokanazo na mazao ya kilimo pamoja na kilimo chenyewe, kwa kuwajengea uwezo pamoja na kuondoa vikwazo vya kijamii katika masuala ya umiliki wa ardhi, ili kuwawezesha kufanya kilimo chenye tija na kuongeza mnyororo wa thamani katika kilimo wilayani Babati.

Aidha,kupitia ruzuku hizo, LSF kwa kushirikiana LANGO itaboresha maisha ya wanawake waishio maeneo ya mwambao wa bahari kupitia rasilimali bahari hasa mwani na tango bahari, ambayo ni mazao ya kibiashara yanayozalishwa zaidi na wanawake wengi pembezoni mwa bahari Mkoani Lindi.

Na eneo la mwisho la ruzuku hiyo, LSF kwa kushirikiana na CSP itatekeleza mradi unaojulikana kama ‘Tanzanite Kwa Uchumi Imara wa Mwanamke’ mradi ambao unalenga kuboresha mazingira ya wanawake wajasiriamali kufanya biashara pamoja kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake kwenye mgodi wa Mirerani Mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad