Askofu Dkt.Shoo ataka viongozi wa dini kuacha kununuliwa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 24, 2023

Askofu Dkt.Shoo ataka viongozi wa dini kuacha kununuliwa

 

Njombe
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt.Fredrick Shoo amewataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuacha kufanya dini kuwa biashara kutokana na kuibuka kwa wimbi kubwa la viongozi wa dini na makanisa yenye mlengo wa kibiashara.

Askofu Shoo amebainisha hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na maaskofu pamoja na viongozi wa dini mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa kamati ya dini mbali mbali uliofanyika mjini Njombe.

"Tusifanye dini kuwa biashara na tena kwa kuwa viongozi mnayo nafasi msikubali kutumiwa na watu wenye nia mbaya,msinunuliwe ninaomba tutunze na kujenga uaminifu unaotakiwa"amesema Dkt.Shoo

Naye mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa wito kwa watanzania kuwa makini na mahubiri yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa dini kwenye vyombo vya habari kwa kuwa yamekuwa ni kinyume na biblia.

"Ukiangali kwenye TV ipo miujiza inayoonyeshwa ambayo inaweza ikapumbaza wananchi na ikatengeneza migogoro, haiwezekani tumekuwa na watu ambao wanasema kwa kuona kwenye TV nimepata muujiza wa kupata gari ni lazima watu wahubiriwe kufanya kazi"Amesema Anthony Mtaka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad