Naibu Mkurugenzi
wa Halotel Bw; Bui Van Thang akikabidhi Mfano wa funguo ya gari kwa mshindi mkuu
wa gari mpya aina ya IST Bi. Scolastica Sostenes Haule, kutoka mkoa wa Ruvuma
aliyeshiriki katika Promosheni ya 7bang bang iliyoendeshwa na kampuni ya
Halotel kwa muda wa wiki 10. Hafla ya Makabidhiano ya gari hilo yalifanyika
katika eneo la Palm Village Mikocheni B ambapo pia sambamba na hilo ulifanyika
uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la Halotel. Pamoja nao ni
Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bw. Abdallah Salum ( Kushoto) mme wa Bi
Scolastika (wapili Kulia) na Naibu Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Nagib Ferej (wa kwanza Kulia). Mkurugenzi
wa Biashara Bw: Abdallah Salum mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST
Ms. Scolastica Sostenes Haule, pamoja na mme wake kutoka mkoa wa Ruvuma
kwa pamoja wakifungua gari mara baada tu ya hafla ya makabidhiano rasmi
ya gari hilo yaliyofanyika katika jengo la Palm Village Mall iliyoko
pembezoni mwa Mikocheni B Dar es Salaam.
Naibu
Mkurugenzi wa Halotel Bw; Bui Van Thang pamoja Mkurugenzi wa Biashara
Bw. Abdallah Salum kwa pamoja wakikata utepe leo kuashiria uzinduzi
rasmi wa duka jipya la huduma kwa wateja la Halotel lililoko ndani ya
Palm Village Mall, iliyoko pembezoni mwa barabara ya Mwai Kibaki eneo la
Mikocheni B Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Biashara Bw. Abdallah Salum akiongea na waandishi wa habari katika
hafla ya makabidhiano ya zawadi ya gari mpya aina ya IST kwa mshindi
mkuu Bi. Scolastica Sostenes Haule, kutoka mkoa wa Ruvuma aliyeshiriki
katika Promosheni ya 7bang bang iliyoendeshwa na kampuni ya Halotel kwa
muda wa wiki 10. Hafla ya Makabidhiano ya gari hilo yalifanyika katika
eneo la Palm Village Mikocheni B ambapo pia sambamba na hilo ulifanyika
uzinduzi wa duka jipya na la kisasa la huduma kwa wateja la Halotel.
Pamoja nao ni Mkuu wa Kitengo Cha Huduma kwa Wateja Bw. Patric
Rwegashora (kushoto) na Msaidizi Mku wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja
Bw. Shabani Said (kulia).
****************
– Ni mshindi wa Grand Draw wa promosheni ya 7 bang bang
– Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa jumla ya washindi 143 wa promosheni ya “7 bang bang”
Dar
es Salaam, 05 Januari 2023 – Kampuni ya Mawasiliano nchini ya Halotel
Tanzania PLC leo imekabidhi zawadi kwa mshindi mkuu aliyejishindia gari
aina ya IST Mpya wa draw kubwa ya mwisho ya promosheni ya wateja
iliyokuwa na jina la 7bang bang.
Promosheni hiyo ya “7 bang bang”
iliendeshwa kwa wiki 10 na kuwapa fursa wateja wote wa Halotel ambao
wamekuwa wakiwaunga mkono kwa kutumia huduma zao kwa miaka saba (07) ya
utoaji huduma bora za M.awasiliano hapa nchini. Tangu kuanza kwa
promosheni hiyo ya bahati nasibu zaidi ya washindi 140 wameweza
kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Vocha yenye thamani mpaka laki
moja, Simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televisheni janja
zenye inchi 50.
Akizungumza wakati wa hafla makabidhiano ya gari
jipya aina ya IST Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Bw; Abdallah Salum,
alisema, “Leo hii, tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya
kabisa kwa kushiriki katika shindano letu la promosheni ya 7 bang bang.
Tumeona itakuwa vizuri ikiwa zawadi hii ya gari ikakabidhiwa wakati
tukiwa tunamalizia msimu wa sikukuu” ukiwa sambamba na kuwashukuru
wateja wetu wote kutumia huduma za Mawasiliano kutoka Halotel sambamba
na kuadhimisha miaka 7 kutoa huduma hapa nchini.
Katika tukio hili la makabidhiano, zawadi kubwa kuliko zote ya gari jipya aina ya IST ilikabidhiwa kwa mshindi.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi rasmi gari hilo alisema, Mkurugenzi wa Biashara
Halotel Bw. Abdallah Salum alisema siku ya leo tunayo furaha sana kuweza
kumkabidhi mteja wetu ambaye ni mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST
katika droo kubwa ya mwisho ya promosheni iliyokuwa na jina la 7 bang
bang “Bi Sholastika Sostenes Haule. Napenda kukupa pongezi kubwa sana na
unavyochukua gari lako, ninakuasa kutumia zawadi hii ambayo ni fursa
adimu, katika kupiga hatua kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako.
Hii iwe hatua kwako, kukufanya uendelee kuweka bidii ili uendelee
kupanda zaidi kimaisha.”
Aidha’ Bwana Abdallah Salum, alitumia
fursa hiyo kuwahimiza wateja wao waendelee kutumia mtandao wa
Mawasiliano wa Halotel ambao unaendelea kuwa na ubinifu kuhakikisha kila
mteja anafurahia huduma za mawasiliano kwa ubora wa hali juu kutoka
Halotel.
Kwa upande wake, Bi Sholastika Sostenes Haule
aliishukuru kampuni ya Halotel, na kuwasihi wateja kuendelea kutumia
mtandao wa Halotel na kushiriki katika promosheni zinazotolewa kampuni
ya Halotel ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zinazokuwa
zinatolewa kupitia promosheni hizo.
Sambamba na tukio hilo la
kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi, Kampuni hiyo ilitumia fursa hiyo
kufanya uzinduzi wa duka jipya na la kisasa linalopatikana Palm Village
Mall iliyopo kando ya barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni, Dar es Salaam
ambapo wateja wa Halotel sasa watapata huduma zote za Halotel katika
Duka hilo.
Duka hili lililoboreshwa kwa njia ya kidigitali
litatoa huduma zote zitakazojumuisha huduma ya kusajili laini mpya na
kusalijili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole, ubadilishaji
wa laini kutoka 3G kwenda 4G, Huduma za vocha (elektroniki na
kukwangua) uthibitishaji wa namba za simu, huduma za HaloPesa, bidhaa za
Halotel kama router na huduma zote za ziada na za baada ya mauzo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara Bw Abdallah Salum
amesema “uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa
Halotel wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake
ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa ukaribu na
urahisi zaidi”.
“Tunapenda kuwakaribisha wateja na watanzania
wote kwa ujumla katika duka letu la Halotel hapa Palm Village Mall
kuweza kupata na kufurahia huduma bora za Halotel katika duka hili”
aliongeza Bw. Abdallah.
No comments:
Post a Comment