Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
OFISA
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA),CPA
Nicodemus Mkama amesema Serikali kupitia mamlaka hiyo ina jukumu la
kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kiutendaji kuwezesha
upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharamia shughuli za maendeleo.
Mkama
amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko
wa Uwekezaji wa Pamoja wa Faida (Faida Fund) ambayo ni sehemu ya
maendeleo katika sekta ya fedha hususan masoko ya mitaji hapa nchini.
Katika
hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali huku Waziri, Ofisi ya
Rais - Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama
akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi.
“Masoko
ya mitaji ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji
wa rasilimali fedha za muda mrefu, yaani zaidi ya mwaka mmoja, kwa ajili
ya kugharamia shughuli za maendeleo.
“Fedha za kugharamia
shughuli za maendeleo hupatikana kwa kuuza hisa za kampuni (shares);
hatifungani za kampuni (hatifungani za Serikali na vipande katika
uwekezaji wa pamoja. Hapa nchini, masoko ya mitaji yanaendelezwa na
kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),”amesema
Mkama.
Ameongeza kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika
utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano
2021/22 – 2025/26 unaolenga kujenga “Uchumi Shindani na Viwanda kwa
Maendeleo ya Watu”, mahitaji ya rasilimali fedha za kutekeleza miradi ya
maendeleo ya jamii na uchumi, hususani miundombinu yanaongezeka.
Amefafanua
ili kufanikisha azma hiyo kunahitajika uwepo wa bidhaa nyingi katika
masoko ya fedha, ikiwa ni pamoja na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kama
Faida Fund. Aidha, uwepo wa bidhaa nyingi katika masoko ya mitaji
unachangia utekelezaji wa Sera za Ukwasi katika Uchumi.
Pia
kuongezeka kwa akiba hapa nchini; kupanuka kwa uwekezaji unaoleta
ongezeko la ajira; Mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali na kuinua kipato
cha watanzania kwa ujumla huku akifafanua Oktoba 17 2022, (CMSA
ilidhinisha Waraka wa Matarajio na Mkataba wa kuendesha Mfuko wa Faida.
“Idhini ilitolewa na CMSA baada ya Watumishi Housing Investments
kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya
Sheria za Tanzania; na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya
uanzishaji na uendeshaji wa Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.
“Faida
Fund ni mfuko ambao umekidhi matakwa ya Sheria, Kanuni na Miongozo ya
Uwekezaji wa Pamoja. Faida Fund ni mfuko unaoendeshwa na taasisi ya
Watumishi Housing Investments (WHI) ambaye ni Meneja wa Mfuko (Fund
Manager) na Benki ya CRDB ambaye ni Mtunza Dhamana wa Mfuko (Custodian).
“Lengo kuu la Mfuko wa Faida Fund ni kuhamasisha wawekezaji wadogo, wa
kati, na wakubwa kuunganisha nguvu zao na kuwekeza kwa pamoja ili
kunufaika na fursa zinazopatikana katika sekta ya fedha.Malengo ya Mfuko
wa Faida ni kuwawezesha watanzania kunufaika na uwekezaji katika masoko
ya fedha.”
Akieleza zaidi amesema mauzo ya vipande katika Mfuko
wa Faida Fund yalifunguliwa Novemba 1,2022 na kufungwa Desemba 31,
2022.Kiasi cha fedha Sh. bilioni 12.95 kimepatikana, ikilinganishwa na
Sh. bilioni 7.5 zilizotarajiwa kupatikana, sawa na mafanikio ya asilimia
173.
Aidha mafanikio hayo yametokana na mazingira wezeshi
yanayotolewa na Serikali kupitia CMSA) ambayo imeidhinisha kushusha
kiwango cha chini cha ushiriki katika uwekezaji wa Mfuko wa Faida Fund
kutoka Sh. milioni moja hadi Sh.10,000 na na hivyo kuwezesha ushiriki wa
wawekezaji katika Mfuko wa Faida Fund, ikiwa ni pamoja na wananchi
wenye vipato vya chini, kati na vikubwa, taasisi na kampuni.
Pia
mazingira wezeshi yanayotolewa na Serikali yamekuwa na matokeo chanya
katika maendeleo ya sekta ya fedha, hususan masoko ya mitaji ambapo
thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji imeongezeka kwa asilimia
8.1 na kufikia Sh.trilioni 34.01 katika kipindi kilichoishia Desemba
2022, ikilinganishwa na Sh.trilioni 31.42 kipindi kilichoishia Desemba
2021.
Thamani ya uwekezaji katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja
imeongezeka kwa asilimia 63.86 na kufikia Sh. trilioni 1.22 katika
kipindi kilichoishia Disemba 2022, ikilinganishwa na Sh.bilioni 744.93
katika kipindi kilichoishia Disemba 2021.
Kwa mantiki hii, leo
unapozinduliwa Mfuko wa Faida Fund, Jumla ya thamani ya uwekezaji katika
Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja itafikia Sh. trilioni 1.35, na jumla ya
thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji itafikia Sh.trilioni 34.14.
No comments:
Post a Comment