HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 5, 2022

WAZIRI WA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA DKT. KIJAJI MGENI RASMI 'VIPODOZI DAY'

 

Mwanchama muasisi wa TCA ambaye pia ni Meneja Masoko wa Buchi Herbal Products, Ally Kubuli  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 5, 2022 amesema kuwa ataonesha  bidhaa za aina mbalimbali siku hiyo ya Vipodozi Day.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa TCA aliyezungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa TCA  Shekha Nasser hayupo pichani katikati  ni Mshauri wa Masuala ya Biashara Sophia Mwaniwa Chamzinga  na  Mtaalamu wa Ngozi Mariam Sabo  kutoka Papilon& Ovio. Mdhamini Mkuu  Lavy.

Na Khadija Kalili
WAZIRI wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara,  Dkt. Ashatu Kijaji (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maonesho ya Vipodozi Day yatakayofanyika Desemba 10, 2022  kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Yamesemwa hayo leo asubuhi Desemba 5, 2022  Jijini Dar Es Salaam katika mkutano na Waandishi wa Habari hawapo pichani ambapo Mshauri wa Chama Cha urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) Jane Consalves ambaye ameongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa TCA Shekha Nasser.

Amesema kuwa wanatarajia wadau zaidi ya 100 watakuwepo Leaders Club kuonesha bidhaa zao sanjari na kutoa huduma na ushauru kwa ujumla.

Amesema kuwa siku ya vipodozi ni tukio linalofanyika maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii matumizi ya kanuni na viambato salama vya vipodozi.

"Siku hii ni mubimu kwa kila kitu kuanzia kutafuta viambato hadi mbinu za uzalishaji vipodozi, watoa huduma wenye weledi watakuwepo ikilenga kuwajali watumiaji vipodozi na shauku ya kuvumbua zaidi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Aidha maadhimisho ya siku hiyo yanahimiza uzalishaji wa bidhaa za urembo zilizo safi, salama na endelevu kuanzia katika hatua za awali hadi kufikia mwisho wa matumizi yake pia maadhimisho hayo yatatoa elimu kwa watumiaji juu ya umuhimu wa kutafuta machaguo bora ya bidhaa, huku akihimiza jamii kubadilika katika matumizi ya bidhaa za urembo na usafi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad