HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 15, 2022

WANANCHI WALIOVAMIA MSITU WA KUNI WILAYANI MVOMERO WATAKIWA KUONDOKA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi kuhusu uvamizi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu uvamizi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwassa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa mkutano na wananchi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ikiwa ni ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi waliovamia Msitu wa Kuni na kuanzisha shughuli za ujenzi wa nyumba, kuacha mara moja na kuondoka katika eneo hilo la hifadhi .

Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

“Sasa tunachowaomba kwanza kusimamisha ujenzi kwenye eneo la msitu ,pili tutaangalia wale ambao wamejimilikisha maeneo makubwa lazima tuyagawe kwa sababu wote ni wavamizi” amesisitiza Mhe. Masanja.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma yake aliruhusu eneo la msitu limegwe jumla ya hekta 2000 ambazo zitagawiwa kwa wananchi lakini wananchi wameendelea kulivamia eneo la msitu.

“Mwaka jana tukaelekeza wananchi wapangwe kwenye hekta elfu 2000 na hiyo ni huruma ya Mheshimiwa Rais Samia kwanza naomba tumpongeze mama yetu ana huruma kwa sababu ilikuwa muondolewe lakini akasema hapana hawa ni wananchi wangu wapangwe” Mhe. Masanja amefafanua.

Ameweka bayana kuwa wananchi waliomo kwenye hekta elfu 2000 zilzizogawiwa wako kihalali na watapimiwa ardhi na kupewa hati zao lakini waliovamia wanapaswa kuondoka katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Masanja amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngombo Wilayani Malinyi, kuhifadhi mazingira na kuacha tabia ya kukata miti hovyo kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad