WAFANYAKAZI WA AIRTEL WAKUNWA VILIVYO NA MSANII DIAMOND NA JOTI,WAFURAHIA MAFANIKIO YAO KWA MWAKA 2022. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 9, 2022

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WAKUNWA VILIVYO NA MSANII DIAMOND NA JOTI,WAFURAHIA MAFANIKIO YAO KWA MWAKA 2022.

Msaani wa Bongo Fleva Diamond Platinum pamoja na mchekeshaji maarufu kwa jina la Joti ambao ni mabalozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, jana walijiunga na wafanya kazi wa kampuni ya Airtel kwenye sherehe za kuanga mwaka ambazo zilifanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya wafanya kazi wake.

Kwenye sherehe hizo, wasanii Hao walitoa burudani ya kutosha na kuwapagawisha wafanyakazi hao wa Airtel.

Akizungumza mara baada ya sherehe hizo, msanii Diamond aliwashukuru uongozi wa Airtel kwa kumpa heshima ya kualikwa na kuwa pamoja kwenye sherehe hizo za kufunga mwaka.

'Ninayo furaha na heshima kwa uongozi wa Airtel kwa kunichangua kuwa balozi wa kampuni yao, lakini pia nawashukuru sana kwa kunialika na kuwa na nyinyi hapa kwa siku Leo. Tupo wasanii wengi lakini mkaona ya kwamba nafaa kushiriki nanyi, nawashukuru sana' alisema Diamond.

'Nimekuwa balozi kwa huduma na bidhaa za kampuni ya Airtel. Naomba kuwahidi kuwa nitaendelea kuwa mfano ili kuendelea kuiweka Airtel kuwa kampuni namba moja hapa nchini kwa huduma za simu za mkononi' aliongeza Diamond.

Akizungumza kwa niaba ya wafanya kazi wa Airtel, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Dinesh Balsighn  alisema kuwa Airtel inathamini sana mchango wa wafanya kazi wake na ndio maana imeandaa sherehe hizi ill kuwakutanisha pamoja na kusherekea mafanikio ya mwaka 2022.

'Bila wafanyakazi hawa tusingekuwa tunafurahia mafanikio ya mwaka 2022. Juhudi zetu ndio zimefanya Airtel kuwa hapa ilipo. Tutaendelea kudhamini juhudi hizi ili kuendelea kukua kwa pamoja' Balsingh alisema.

'Nachukua fursa hii pia kuwashukuru mabalozi wetu Diamond na Joti kwa kukubali mwaliko wetu na kuja kujumuika nasi hapa Leo. Tumefurahi pamoja na kwa kweli tumeona mafanikio Kupitia kwenu na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwa siku za mbeleni, aliongeza Singano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad