HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2022

WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI WATEMBELEA ENEO LA VIWANDA LA SINO TAN KIBAHA MKOANI PWANI

Meneja Masoko wa Mradi wa Viwanda wa Sino Tan (Sino Tan Industrial Park), Chawn akizungumza na wafanyabiashara wa nchi mbalimbali waliotembelea katika Mradi wa Eneo la Viwanda lililopo Kwala Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Samawati Capital Partiners, kutoka Nchini Kenya, Samwel Ndonga akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea eneo la Viwanda la Kwala Kibaha Mkoani Pwani Desemba Mosi, 2022 kwaajili ya kuangalia fursa zilizopo katika uwekezaji katika eneo hilo.
Mfanyabiashara wa Nchini Uturuki na Mkurugenzi wa Smart Power, Kaan Ozkan akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2022 mara baada ya kutembelea Eneo la Viwanda lililopo Kwala Kibaha Mkoani Pwani.
Mshauri wa Teknolojia, kutoka Wizara ya Uwekezaji ya Nchini Gabon, Jeff Didier Mkurugenzi wa Samawati Capital Partiners, kutoka Nchini Kenya, Samwel Ndonga akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea eneo la Viwanda la Kwala Kibaha Mkoani Pwani Desemba Mosi, 2022 kwaajili ya kuangalia fursa zilizopo katika uwekezaji katika eneo hilo.
Msimamizi wa Mradi wa Sino Tan, Mhandisi Alexander Nchaholuli, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya wadfanyabiashara na wawakilishi wa nchi mbalimbali kutembelea eneo la Mradi wa eneo la Viwanda lililopo Mkoani Pwani.
Baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji waliotembelea eneo la Viwanda la Sino Tan lililopo Mkoani Pwani wakipata maelekezo kutoka kwa meneja masoko wa Sino Tan Industrial Park, Chawn.

WAWEKEZAJI na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali watembelea mradi wa eneo la Viwanda la Sino Tan (Sino Tan Industrial Park) lenye ukubwa wa hekari 2,500 lililopo Kwala Kibaha Mkoani Pwani.

Mradi huo unalenga kuajiri watanzania zaidi ya 100,000 huku ukiwa umegharimu dola za Marekani 150.

Mshauri wa Teknolojia, kutoka Wizara ya Uwekezaji ya Nchini Gabon, Jeff Didier akizungumza leo Desemba Mosi, 2022 walipotembelea eneo la mradi huo, amesema hakutarajia kuona uwekezaji mkubwa unaofanyika katika eneo hilo la Mradi wa Viwanda, Serikali ya Gabon wataangalia ni Sekta gani wataweza kuwekeza katika Mradi wa viwanda wa Sino Tan Kibaha.

Amesema Umoja wa Nchi za Afrika wanatakiwa kuangalia namna ambayo wanaweza kuwekeza katika mradi huo.

Amesma kama Mwakilishi wa nchi ya Gabon anashauku ya kuja kuwekeza katika Vifaa ya umeme na Teknolojia.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Samawati Capital Partiners, kutoka Nchini Kenya, Samwel Ndonga amesema kutembelea katika eneo la Mradi huo la wamekuja kuangalia fursa zilizopo katika uwekezaji kwani tayari hapa nchini wamewekeza kwenye Kilimo na katika eneo la Uchakataji wa Chakula.

Amesema Mradi huo wa Kibaha utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na watanzania wote kwa kujipatia Ajira za muda mfupi na mda Mrefu.

Akizungumzia kuhusiana na matarajio yake Ndoga amesema kuwa wanasubiri Mradi huo ukamilike ili waanze kuzungumza na kampuni za nchini Kenya zinazoweza kuja kuwekeza.

Mfanyabiashara wa Nchini Uturuki na Mkurugenzi wa Smart Power, Kaan Ozkan amesema kuwa Mradi huo wa Viwanda Kibaha ni fursa kwa kuwekeza katika Viwanda pamoja na nishati.

Amesema Kama Mwekezaji kwenye nishati pia ni fursa kwa kila Mtanzania kupata nishati ya Umeme popote alipo.

Kwa upande wa Msimamizi wa Mradi wa Sino Tan, Mhandisi Alexander Nchaholuli, amesema mradi huo watauendeleza katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wataendeleza Ekali 1,000 na awamu ya pili wataendelea Ekali zilizobaki kwa miaka mitatu.

"Kwahiyo tunategemea baada ya ya viwanda 212 kukamilika kutakuwa na mapato ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni sita kwa mwaka. "

Amesema Sino Tan wanashirikiana kwa karibu na serikali katika kutekeleza Mradi huo, ambapo katika kutekeleza mradi lazima baadhi ya miundombinu inafikishwa na Serikali kwaajili ya maendeleo ya Mradi huo.

Amesema katika Mradi huo serikali imewezesha kufikika katika eneo hilo kwa kutengeneza barabara, Umeme tayari umefika, na Wafanyakazi wa Dawasa tayari wameshapeleka maji.

Amesema Utekelezaji wa Mradi huo tayari wameshaandaa eneo, wameanza kuchonga barabara na tayari lango la Kuingilia pamoja na Ofisi zinatarajiwa kumalizika kujengwa Machi, 2023.

Ziara hiyo iliratibiwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara(MIIT).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad