HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 7, 2022

Tanzania na Zambia wakutana kujadili usalama wa bomba la mafuta


Waziri wa Ulinzi Nchini Zambia Ambrose Lufuma akizungumza kuhusiana na mikakati ya ulinzi wa bomba la mafuta ya Dizeli kwenda nchini Zambia yakitokea nchini Tanzania. 

Waziri wa Nishati Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana usafirishaji wa mafuta ya Dizeli kwenda nchini Zambia mara baada kikao kati ya Tanzania wa Zambia kwa Wizara za Nishati, Ulinzi na Mambo ya Ndani , jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhandisi Peter Kapala akizungumza kuhusiana na makubaliano ya utekelezaji wa Bomba la Mafuta ya Dizeli kwenda nchini humo.
Picha mbalimbali za mkutano wa kujadili usalama wa bomba la mafuta ya Dizeli  kutoka Tanzania kwenda Zambia.

*Tanzania kunufaika na Uuzaji wa Gesi nchini Zambia
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI ya Tanzania na Zambia yapitisha mapendekezo ya kuimarisha ulinzi wa bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA) ya usafrishaji wa mafuta ya dezeli na kuachana na usafirishaji wa mafuta ghafi yasiosafishwa.

Ulinzi huo unakwenda kutokana na usafirishaji huo unaweza kuhujumiwa na wananchi kwani hayo mafuta yakitolewa kwenye bomba yanakwenda katika matumizi tofauti na usafirishaji wa mafuta ghafi yasiosafishwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema nchi ya Tanzania na Zambia zina mradi wa muda mrefu ulioanzishwa na Marais Waanzilishi wa nchi zote mbili Keneth Kaunda na Rais Julius Kambarage Nyerere kuanzisha bomba hilo la mafuta.

Amesema katika kufanya ulinzi huo kutakuwa na walinzi kwanza na kufatia teknolojia mbalimbali ikiwemo Drone na Kamera za CCTV pamoja na elimu ya ulinzi kwa wananchi wanaopitiwa na bomba hilo kuwa sehemu ya ulinzi.

Pia nchi hizo zimekubaliana kuweka ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo hayo yaliyotolewa na Wataalam wa nchi zote mbili, ndani ya siku 45 yawe yametekelezwa

Makamba alisema miaka ya nyuma Bomba hilo la mafuta lilikuwa linasafirisha mafuta ghafi yasiyosafishwa na kuelekea nchini Zambia ambapo huko kuna mtambo wa kuyasafisha mafuta hayo ili yawe mafuta safi na kuwa tayari kwa kutumia katika magari na mitambo mingine.

Makamba amesema Kutokana na maendeleo ya uchumi kati ya nchi mbili na Teknolojia kukua Serikali ya Zambia iliamua kubadilisha bomba la TAZAMA kuacha kusafirisha mafuta ghafi na kutaka kuanza kusafirisha mafuta ya diseli na kutokana na hali hiyo walianza kufanya manunuzi ya kuwezesha bomba hilo kubadilishwa na imechukua gharama kubwa.

‘’Usafirishaji wa mafuta ya diseli kwa njia ya bomba kunahitaji usalama wa bomba hilo kuwa mzuri na kuwa makini nalo kwa sababu mafuta yale ghafi ni mazito machafu ambapo hata kama mtu akiiba kwa kuchepusha bomba hawezi kuyafanyia chochote tofauti na haya ya Diseli ambayo iko safi ,’’amesema Januari

Amesema bomba litakapochokonolewa na watu kuchepusha mafuta hayo ni hatari kubwa hivyo nchi zote tumeamua kufanya utaratibu wa usalama wa bomba na kutembelewa na na Mawaziri Waziri wa Nishati wa Zambia,Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya ndani wa Zambia pamoja na wataalamu wao wakiwemo makatibu wakuu wa wizara hizo na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi mbili kujadili kwa kina juu ya usalama wa bomba hilo na kutoa mapendekezo yatakayotuongoza katika kufanikisha jambo hilo.

Amesema hatua ya Zambia kubadilisha matumizi ya bomba hili kutoka kutumika kusafirisha mafuta ghafi hadi kufikia mafuta ya Diseli ni maamuzi makubwa na ya msingi na kufanya Tanzania kuendelea kuwa soko na njia ya kuhakikishia Zambia kuwa na usalama wa mafuta na Bandari kutumika.

Kwa Upande wake Waziri wa Nishati nchini Zambia,Eng Peter Kapala aliishukuru Serikali ya Tanzania katika mkutano huo na kusema kuwa ni muhimu kutekeleza mapendekezo hayo kwa muda waliojiwekea.

Alisema ni jukumu la nchi zote mbili kuhakikisha usalama unakuwepo katika bomba hilo ili kusiweze kutokea kwa uharibifu wowote na kuhakisha uimarishaji wa ulinzi.

Waziri wa Kapala amesema mbali na bomba hilo pia wanatarajia kununua gesi kutoka nchini Tanzania kwa kuwa na bomba lingine tena kutokana kuweka na uharibibifu wa mistu yanayochangiwa na matumizi nishati ya kuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad