TANTRADE YAIFUNGULIA MILANGO TCA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 11, 2022

TANTRADE YAIFUNGULIA MILANGO TCA


Mwenyekiti wa TCA na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akizungumza leo Desemba 10, 2022 uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Na Khadija Kalili 
 MKURUGENZI Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis amesema kuwa kuwa kuanzia sasa serikali itafanya kazi na Chama Cha Vipidozi Tanzania (TCA) ikiwa ni katika kuhakikisha wanalinda afya za watumiaji wa vipodozi na sekta ya urembo na watanzania wote kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leo Desemba 10, 2022 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji. 

Amesema enzi za kupenda na kithamini vipodozi au bidhaa kutoka nje ya nchi zimepitwa na wakati. "Hivyo nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa Tamasha hili la aina yake huku nikiwataka muongeze kasi katika uzalishaji wa vipodozi visivyo na viambata vyenye sumu na nina waahidi kuwa Tantrade tutawapa fursa ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.

Nawakaribisha TCA mtukimbilie muda wowote na milango iko wazi kwa ajili yenu huku nikiwaahidi kuwa tutawatafutia masoko nje ya nchi kwani hii ni fursa kubwa katika kuitangaza nchi kimataifa katika nyanja ya biashara pia kuanzia mwakani tutawapa fursa ya kuonesha bidhaa zenu kwenye maonesho ya Viwanda Tanzania pamoja na makongamano mbalimbali ya biashara kwa kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa kupitia muamvuli wa TCA."

"Tasnia hii ya vipodozi ina wigo mpana ambao umeongeza ajira na kukuza uchumi kwa vijana na kinamama wa hapa nchi, Wanawake shikamaneni na mnyanyuane kiuchumi ikiwa ni kwenye kuongeza kipato katika familia zenu.  Amesema Latifa Khamis 

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser ameweka wazi kuwa inaonesha kuwa wanawake wengi hasa wakaazi wa Wilaya ya Kinondoni ni wahanga wa kunyonyoka kope kutokana na kubandika  kope za bandia huku wakitumia gundi ambazo zimewapatia madhara.

Pia amewaasa wanawake kujenga Utamaduni wa kutumia vipodozi vya asili visivyo na madhara huku akisema endapo watatumia mafuta ya mnyonyo yanayoyengenezwa ni mwanachama wao Nzalakado yatasaidia kuziotesha kope hizo. Bi Shekha ameiomba serikali iweze kuwapunguzi kodi kwenye bidhaa za urembo ikiwemo saluni na kuwekwe muongozo ambao utakua ni rafiki kwenye kulipa kodi kwa kupitia chama hicho TCA kilizinduliwa miaka mitatu iliyopita Jijini Dar es Salaam ambao ni muunganiko wa wadau wenye kuuza na kutengeneza vipodozi nchini.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis akizungumza leo Desemba 10, 2022 alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji. 
Mwenyekiti wa TCA na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akizungumza leo Desemba 10, 2022 uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakitembelea mabanda kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakipata maelekezo walipotembelea mabanda kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Picha za pamoja katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad