HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 16, 2022

Katondo: Ahamasisha Uridhiaji wa Mkataba wa IMO Katika Utunzaji wa Mazingira ya Bahari

Mkurugenzi wa Usalama na mazingira wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stella Katondo akizungumza na waandishi wa habari  mara baada kufunga mkutano wa siku Tatu wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa mkutano wa nchi wanachama wa nchi 15 wa Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) Tanzania ikiwa mwenyeji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkurugenzi wa  Usalama na mazingira wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stella Katondo   mara baada kufungwa mkutano wa siku Tatu wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa Bahari 
kutoka nchi 15 wakiwa kwenye warsha ya siku tatu wakijadili itifaki ya usimamizi wa habari na mazingira.
Picha pamoja ya wadau wa bahari na Mgeni Rasmi mara mara baada ya kufunga warsha ya siku tatu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Katondo:ahamasisha uuridhiaji wa mkataba wa IMO katika utunzaji wa mazingira ya bahari


*TASAC yasema mkataba uko katika kukuza uchumi wa bahari

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NCHI mwanachama 15 za Afrika zimeshiriki katika mkutano wa kukuza uelewa wa pamoja juu ya Mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari juu ya maji yanayokuwa katika meli yazimwagwe bila kufuata utaratibu wa uhifadhi wa mazingira.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Usalama na mazingira wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo akizungumza wakati akifunga Warsha wa nchi wanachama zilizoshiriki katika kujadili mkataba wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) unaohusiana na maji yanayokuwa ndani ya Meli yasomwagwe bila kufuata utaratibu ikiwa ni kutunza mazingira na viumbe hai katika nchi ambayo Meli imefika uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Katondo amesema kuwa Mwitikio wa nchi mwanachama umekuwa mkubwa na ni jambo ambali dunia imeanza kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwaajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyozaliwa majini vinakuwa hai ambapo kazi ya nchi hizo ni kuhamasishana katika kuuridhia.

Katondo amesema kuwa mkutano huo Tanzania ndio ilikuwa mwenyeji hivyo katika kuadhimia ni kila nchi kuangalia namna ya kuridhia mkataba ambao kimsingi hauna ubaya katika utunzaji wa mazingira ya uoto na vizazi vilivyomo na vijavyo. katika bahari.

"Ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka na inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kwani kwa sababu ya viumbe ambavyo vinafanyika kuwa uchumi vitapotea pamoja na vyombo vya usafiri majini vitaharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa."

Amesema kuwa mkutano huo utatilia mkazo wa uridhiaji wa itifaki ya sheria ya bahari kwaajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.

Katondo amesema kuwa maji yanabebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo pia ikiwa na mzigo mdogo yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na Maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.

"Maji hayo yana viumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi wataleta namna tofauti ya kimazingira Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) liliona umhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa, kinachotakiwa ni kuto kumwagwa baharini kama nchi mwanachama wa IMO tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwagwa katika kati ya habari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji.

Amesema Kwa Tanzania Sasaivi tupo katika hali nzuri kwa sababu tumeshaanza kuridhia mkataba pia amesema Kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu. Na mpaka sasa wameshaanza kupokea maoni yao.

Washiriki wa mkutano huo ni Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bandari, Taasisi ya Bahari ya Dar es Salaam (DMI) wa wawakilishi wa Nchi 14 za Afrika

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na Maji yanayotokana na uchafunzi wa vyombo vya Usafiri Majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.

Amesema kuwa Rais Dk.Samia Hassan Suluhu amefungua mipaka ambapo sasa tunakwenda katika uchumi wa Bluu ambao suala mazingira ya bahari lazima yaangaliwe kwani inawezekana kuna viumbe ambavyo vinazaliwa na ndani maji yaliyokuwa kwenye meli hakishushwa baharini katika maji ya kitaifa au eneo lolote la bahari kuna uwezekano wa kushushwa na viumbe ambao wamezaliwa baada maji kukaa kwa muda mrefu mara baada ya kushusha kuharibu viumbe wengine wa asili.

Mkeyenge maji yakishushwa yanaweza kuzalisha viumbe wengine ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uendelevu viumbe ambao wapo baharini na tunaowahitaji.

Amesema uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi na kufikia uchumi wa bluu kama mikataba hii hatutairidhia na kuzingatia ni jinsi gani tunaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa.

Shirika la Kimataifa la Bahari linatoa elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya usafiri kwa njia ya maji, taasisi zinazohusika na masuala ya bahari zimeshiriki warsha hiyo ili kuwa na uelewa wa pamoja ili mkataba utakaporidhiwa na kutengeneza kanuni za Kutumika hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad