HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 5, 2022

Kampuni ya Letshego yasaidia vifaa tiba kitengo cha watoto hospitali ya Taifa Muhimbili vyenye thamani ya sh milioni 50/=

 
Na Mwandishi wetu


Kampuni ya Letshego Holding imesaidia vifaa tiba kwa kitengo cha wagonjwa watoto wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili vyenye thamani ya Sh milioni 50.

Vifaa tiba vilivyokabidhiwa kwa kitengo hicho vifaa sita vya kusimamia mwenendo wa moyo (Cardiatric Monitor), mashine 20 za kidigitali za kupima shinikizo la damu (BP Mashines), vifaa 18 vya kupima uzito (Weight scale) na vipima joto 10 au Ifra-Red thermometer.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Letshego Holding Limited Philip Odera ambaye alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kushiriki katika masuala ya kijamii.

Bw. Odera alisema wanajisikia fahari kubwa kusaidia sekta ya afya na hasa kitengo hicho muhimu cha wagonjwa watoto huku akisisitiza kuwa suala la afya ni jambo muhimu sana kwa jamii kwani ndiyo chanzo cha kufanya shughuli yoyote.

Alisema kuwa shughuli zote za taasisi hiyo ni kusaidia kuboresha maisha ya watu, hivyo kusaidia kitengo cha tiba kwa watoto ni moja ya njia ya kutekeleza jukumu lao.

Alifafanua kuwa maana kubwa ya neno Letshego kwa lugha ya Setwana kutoka nchi ya Botswana ni msaada, jambo ambalo limewalazimu kutimiza wajibu wetu kwa jamii kwa kusaidia msaada huo.

“Shughuli zetu kubwa ni kusaidia kuinua maisha ya watu na sekta ya afya ndiyo nguzo kubwa katika ustawi wa jamii. Msaada ni wa kusaidia kizazi kijacho ambacho ndicho kitaendeleza sekta mbalimbali,” alisema Odera.

Alifafanua kuwa Letshego inajivunia kuwekeza hapa nchini na katika nchi nyingine barani Afrika na wanafanya vizuri katika sekta ya fedha na hivyo kuinuakipato kwa jamii.

“Msaada huu ni jukumu letu katika jamii ambayo ndiyo wateja wetu katika shughuli zetu za kila siku. Jamii ina hitaji kubwa la matibabu jambo ambalo taasisi yetu imelipa kipaumbele na kwa kuanzia tumeona tusaidie vifaa tiba katika kitengo hiki cha tiba kwa watoto, ” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi alisema msaada huo ni muhimu sana kwa hospitali yao ambayo inatibia takribani wagonjwa 2000 kwa siku.

Profesa Janabi alisema kuwa hospitali ya Muhimbili ni miongoni mwa hospitali kubwa kwa nchi za Afrika Mashariki na imepanua wigo wa tiba kwa sasa.

“Ni Msaada mkubwa na unahitaji pongezi kubwa pia. Tuna uhitaji wa vifaa hivi kwani ni muhimu kwa tiba nyingi. Naipongeza Letshego Holding kwa kusaidia na tunawaomba waendelee kutusaidia,” alisema Profesa Janabi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt Radhid Mfaume aliipongeza kampuni ua Letshego Holding kwa msaada huo na kuomba waendelee kufanya hivyo kwani wanawasaidia Watanzania.

“Huu sasa ni muunganiko ambao naomba uendelee. Taasisi au kampuni inayosaidia vifaa tiba ina lengola kujenga jamii yenye afya. Nawaomba Letshego iendeleze msaada huu,” alisema Dkt Mfaume.


Mwenyekiti wa kampuni ya Letshego Holding Limited Philip Odera ( wa pili kushoto) akizungumza wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 50 kwa kitengo cha watoto cha hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume na kushoto ni kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Letshego, Aobakwe Aupa Monyatsi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume (wapili kulia) akizungumza wakati wa hafla maalum ya kupokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Sh milioni 50 kutoka Kampuni ya Leshego Holding Limited kwa ajili ya Kitengo cha watoto cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati wa pili kushoto ni mwenyekiti wa kampuni ya Letshego Holding Limited Philip Odera na wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Letshego, Aobakwe Aupa Monyatsi.


Mwenyekiti wa kampuni ya Letshego Holding Limited Philip Odera ( wa pili kushoto) akikabidhi kifaa maalum kinachotumika kupima mwenendo wa moyo (Cardiatric Monitor) kwa mganda mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume ( wa pili kulia). Wa kwanza ni Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Letshego, Aobakwe Aupa Monyatsi. Katika hafla hiyo, kampuni ya Leshego Holding Limitedalikabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa Kitengo cha watoto cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili vyenye thamani ya Sh milioni 50.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika Microfinance Tanzania, Bw. Baraka Munisi akizungumza wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 50 kwa kitengo cha watoto cha hospitali ya Taifa ya MuhimbiliViongozi mbalimbali wa wa kampuni ya Letshego Holding Limited, Taasisi ya kifedha ya Faidika, benki ya Letshego na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume (wa tatu kulia waliokaa) mara baada ya kumaliza kwa hafla maalum ya kukabidhi vifaa tiba vyenye Sh milioni 50.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad