HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 5, 2022

Equity Bank Tanzania imemteua Bi. Isabela Maganga kuwa Mkurugenzi Mtendaji

Benki ya Equity Tanzania, kampuni tanzu ya Equity Group Holdings Plc imemteua Bi. Isabela Maganga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki. 

Bi. Isabela ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Fedha na Uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Coventry, Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Mazingira na Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. 

Pia ana Diploma ya Juu ya Benki kutoka Shule ya Biashara ya Milpark. Bi. Isabela ni mtaalamu wa Benki na aliyebobea kwenye masuala ya kifedha ya wafanyabiashara wadogo na wa kati. 

Ana uzoefu mkubwa katika benki ya biashara, akiwa amehudumu katika tasnia ya fedha kwa miaka 16. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania na awali Mkuu wa Kitengo cha Biashara katika Benki hiyo. 

Akizungumza wakati akimkaribisha Bi. Maganga katika nafasi yake mpya, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Equity Tanzania, Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema, “Tunafuraha kutangaza kumteua Bi. Isabela Maganga kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki. 

Ujuzi wake dhabiti na uzoefu utakuwa muhimu tunapoendelea na mipango yetu ya kukuza Benki na kuhudumia watu zaidi kulingana na madhumuni yetu ya kubadilisha maisha, kutoa heshima na kupanua fursa za uzalishaji mali. 

Akizungumzia uteuzi huo, Bi Maganga alisema, “Ninashukuru kwa kuheshimiwa kupata nafasi ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania na kuongoza timu imara ya watu wenye vipaji na wataalamu wa sekta hiyo. 

Tunapoendelea kutembea katika safari ya kubadilisha maisha ya watu wetu, nathibitisha kujitolea kwangu kuendelea na kazi ambayo tumekuwa tukifanya, kuwahudumia wateja wetu vyema na kuwaunga mkono katika ukuaji wao. Bodi ya Wakurugenzi inampongeza Bi. Maganga kwa kuteuliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad