HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 10, 2022

WAZIRI MABULA ASITISHA VIBALI VYA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA

 

Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nyumba na Makazi akiongea na vyombo vya Habari leo Jijini Dodoma kuhusu maagizo yake ya kusitisha ujenzi holela wa vituo vya mafuta na kanununi za mipango miji.

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula amesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo kwa muda wa miezi mitatu kuanzia sasa.

Waziri ametoa agizo hilo ili kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi na Wizara zinazohusika na utoaji vibali kufanya tathimini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta kufuatia kuwepo kwa ujenzi unaokiuka maelekezo ya mipango kabambe iliyopo.

Waziri Mabula ametoa agizo hilo leo tarehe 10, Novemba 2022 mbele ya vyombo vya habari Jijini Dodoma nakuongeza kuwa baadhi ya wamiliki wamekuwa wakiomba vibali vya ukarabati wa majengo chakavu mijini na baadae kufanya uendelezaji wa Maeneo hayo kinyume mipango kabambe iliyopo.

Waziri Mabula aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa kanuni husika, kumekuwepo na hujenzi holela wa vituo vya mafuta nchini usiozingatia matakwa ya Sheria ya Mipangomiji na Kanuni zake jambo linalochagiza uwepo wa agizo hilo la kusitisha vibali hivyo.

Aidha Waziri Mabula ameelekeza kusitisha kutoa vibali vya ujenzi vinavyokiuka Mipango kabambe wa Majiji, Manispaa, Miji na kusitisha ugawaji viwanja kiholela unaopelekea taswira ya miji yetu kuharibika akisisitiza kuwa kama kuna mpango wa kujenga magorofa eneo husika ufuatwe mpango uliopo.

Aidha Dkt. Mabula amezitaka mamlaka za upangaji kuhakikisha uendelezaji upya maeneo ya ndani ya miji na mgawanyo wa maeneo unaofuata Mipango Kabambe iliyopo na mipango kina iliyoandaliwa.

Waziri Mabula amewaelekeza wataalamu katika ofisi za ardhi kote nchini zisimamiwe utekelezaji wa Mipango Kabambe na kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha mapendekezo ya mipango hiyo yanatekelezwa.

Waziri Mabula ameitaja sheria ya Mipango miji Sura 355 kupitia fungu 77(1)b kuwa inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, mamlaka ya kutoa kanuni za viwango vya matumizi ya ardhi.

Dkt. Mabula ameitaja Sheria hiyo na kanuni ya 93 ya mwaka 2018 kuwa ndiyo inayotoa maelekezo kuwa umbali wa kituo kimoja hadi kingine ni mita 200 kwa maeneo yaliyopangwa na mita 500 kwa maeneo yasiyopangwa.

Aidha Waziri Mabula amesema tayari Wizara yake imetoa imeidhinisha Mipango Kabambe 26 ikiwemo ya Majiji 6 ya Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tanga pamoja na Mipango Kabambe ya Mikoa ya Iringa, Morogoro, Mtwara Mkindani, Songea, Singida, Tabora, Kigoma Ujiji, Mpanda, Sumbawanga, Bukoba, Shinyanga na Musoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad