Na Avila Kakingo, Michuzi TV
WATANZANIA wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya ya macho mara kwa mara ili kuondokana na upofu
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), leo Novemba 6, 2022, jijini Dar es Salaam. naAfisa kutoka Vision Care,Caren Mashaya amesema kuwa asilimia 80 ya upofu wa macho unazuilika hivyo ni muhimu kupata tiba mapema kwa kuwaona wataalamu.
"Matatizo ya macho yanatibika hivyo iko haja ya kuona umuhimu wa kuwaona wataalamu ili kupata tiba." Amesema
Amesema wananchi wenye umri wa miaka 40 wako kwenye hatari ya kupata presha ya macho hivyo ni muhimu kila mtanzania akaona umuhimu wa kuangalia afya ya macho mara kwa mara.
Akijibu baadhi ya Maswali waliyoulizwa amesema kuwa mtu mwenye tatizo la Mtoto wa jicho lazima afanyiwe uchunguzi na matibabu ili kuweza kupunguza hatari ya kupata maradhi makubwa zaidi.
Wataalamu wa Macho wakiwapima waandishi wa habari Mataitizo ya macho wakati wa Mkutano mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) uliofanyika Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment