Uvuvi haramu changamoto nyingine kwenye mto Ruaha kukauka - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 12, 2022

Uvuvi haramu changamoto nyingine kwenye mto Ruaha kukauka

Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi 'Afande Sele'  akionesha Mtumbwi ulioharabiwa na Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Hili ndo eneo ambalo wavuvi haramu wanaendesha Shughuli uvuvi haramu ambapo kutokana na operesheni imepungua.
Mfuko wa Samaki zilizoharibika zilizotelekezwa wakati operesheni wa Askari wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Ruaha wakati walivyofanya operesheni eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi akizungumza na waandishi habari kuhusiana Uvuvi haramu unaofanyika kwenye Mto Ruaha na Hifadhi ya Ruaha katika eneo la Matopetope-Ikoga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

* Wananchi waingiza mitumbwi na nyavu kwenye hifadhi

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv Mbarali
WAKATI serikali ikiweka mkazo wa kutoendesha shughuli za Uvuvi katika hifadhi imekuwa tofauti kwa wananchi wa Bonde la Usangu/Ihefu kuendesha shughuli hizo ndani ya hifadhi ya Ihefu na Mto Ruaha.

Hali hiyo imebainika baada Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) kutembelea Mto Ruaha kwenye Bonde la Usangu/Ihefu eneo la Matopetope-Ikoga wilaya ya Mbarali mkoani.

Akizungumza eneo la Matopetope ambapo shughuli za Uvuvi zinafanyika Mragibishi na mdau wa Mazingira Seleman Msindi 'Afande Sele' amesema kuwa wananchi kuendesha shughuli za uvuvi ndio chanzo cha kukauka mto Ruaha na kupotea kwa Uoto wa asili bonde la Usangu/Ihefu.

Msindi amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yametokana na shughuli za kibinadamu na kusababisha mto Ruaha kukauka katika kipindi kufupi cha kiangazi.

Amesema kuwa uvuvi haramu kwenye mto Ruaha haukubaliki kutokana na maji hayo yanashughuli za kiuchumi ya kuzalisha umeme kwenye vituo vya Mtela ,Kidantu pamoja na kihansi.

Aidha amesema kuwa wananchi wanaingiza mitubwi na kufanya uvuvi haramu na miti ya mtumbwi imekatwa kwenye hifadhi ya Ruaha Bonde la Usangu/Ihefu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad