HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2022

UPANGAJI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA KUPUNGUZA UKATILI KATIKA JAMII

  

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Same Elisha Kapama  akiwasilisha mpango wa upangaji wa bajeti yenye mlengo wa kijinsia  kuhusu namna walivyoweza kujenga matundu ya vyoo 12 na kuwanufaisha wanafunzi elfu 1213, kujenga mabweni 7 na kuwanufaisha wanafunzi 560, kununua taulo za kike boksi 200 na kuwanufaisha watoto wa kike waliopo mashuleni 803 pamoja na kujenga Zahanati 6 na kuwanufaisha wananchi elfu 11,217. Pia amesema wameweza kupunguza mimba mashuleni kutokana na kutoa elimu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pamoja na RUWASA kwa kujenga miradi ya maji karibu na wananchi ili kupunguza mwendo wa kufuata maji mbali hii yote ikiwa ni mkakati wa kupunguza ukatili wa kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Kishapu Joyce Macha akitoa maelezo kuhusu ongezeko la mimba kutoka asilimia 8 hadi 12 kwasababu ya mwingiliano wa wananchi hasa kwenye mgodi wa Almasi pamoja na kupungua kwa utolo wa wanafunzi mashuleni kutoka asilimia 25.6 hadi 20.1 ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa uandaaji wa Bajeti kupitia kwenye mikutano ya vijiji pia kuwepo kwa mpango wa kujenga mabweni mawili katika Shule ya Sekondari na kujenga kituo cha afya na maji kupitia fedha za wafadhili. Pia amesema kuongezeka kwa mimba mashuleni ni kutokana na umbali wa shule na wanafunzi wanatembea umbali mrefu hivyo wanapata vishawishi mbalimbali wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo kutoka Halmashauri ya Morogoro Vijijini Daniel John  akieleza utekelezaji wa bajeti ya mlengo wa kijinsia katika kupanga na ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji wa Miradi ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya  Mbeya Vijijini Wazidi Mahenge akieleza kuhusu namna walivyofanikiwa kujenga mabweni 60 ili kuboresha Wanafunzi kujisomea mashuleni ili kujikinga na changamoto mbalimbali za ukatili wa kijinsia hasa watoto wa kike pamoja na kutoa elimu ya Uzazi kwa Vijana ili kuepuka ukatili wanapokuwa na familia zao ikiwa na pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika mpango wa maendeleo wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu kutoka Halmashauri ya Muheza Kombo Ibrahimu  akitoa maelezo kuhusu namna wilaya hiyo ilivyoweza kufanikisha kujenga mabweni 5 na kila bweni linawea kuhudumia wanafunzi wapatao 80, kuanza kwa ujenzi wa miradi ya maji 10 hii ni kutokana na changamoto kuwa ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo pamoja na kujenga Zahanati 4 zenye thamani ya shilingi milioni 200 na wanufaika kuwa 6304 hii yote ikiwa ni katika upangaji na utekekelezaji wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakisikiliza uwasilishwaji wa Upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad