HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2022

TGNP YATOA YA MAFUNZO UANDAAJI WA BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA KWA MADIWANI, MAAFISA MIPANGO, MAENDELEO YA JAMII NA WARATIBU WA MADAWATI YA JINSIA

 

Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa maafisa mipango na bajeti, maendeleo ya jamii na waratibu wa madawati ya jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Afisa Programu Idara ya Mafunzo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai akizungumza kuhusu namna Mtandao huo unavyofanya kazi na jamii hasa kwenye uandaaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Lihoya Chamwali akitoa mada kuhusu namna wanavyoweza kuweka usawa wakjinsia pamoja na kuweka bajeti yenye mlengo wa kijinsia kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini leo tarehe Novemba 22, 2022.
Baadhi ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakichangia mada kwenye warsha ya kuwajengea uwezo kuhusu Bajeti yenye mlengo wa jinsia inayofanyika kwa siku nne jijini Dar es Salaam.
Semina ikiendelea 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad