HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 16, 2022

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUHUSU KUSHIRIKI KWENYE NAFASI ZA UONGOZI

 


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeandaa warsha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye vyuo kumi ambavyo ni Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi, IFM, NIT, Mwalimu Nyeere, TIA, Mzumbe, Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo chaMipamgo MNMA, ISW na Chuo cha Maji ambapo vyuo hivi vinapatikana kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

Akizungumza wakati wa kufungu mafuzo hayo ya siku tatu Mkuu wa Idara ya Maarifa, Utafiti na Uchambuzi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Catherine Kasimbazi alipowwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema warsha hii imejikita katika kuongesza ushiriki wa wanafunzi wa kike katika nafasi za uongozi na ngazi mbalimbali za maamuzi kwa kuwaelimisha kuhsu masuala ya uongozi ili waweze kufahamu miongozo, sera na kanuni zinazoongoza Serikali ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Pia amesema mafunzo haya yatawasaidia wale ambao ni viongozi kuendelea kuwa bora zaidi na kuweza kuendesha Serikali zao kwa ushirikiano mkubwa na kuwa chachu ya mabadiliko kiungozi na kuongeza ushiriki wa Wanafunzi wengi zaidi wa kike kushika nafasi za uongozina ngazi za maamuzi.

Kidunia, Takwimu za Interparliamentarian Union (IPU) zinaosesha kuna wanawake 21 ambao wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali na kwa upande a afrika tumewahi kuwa na marais watano wanawake ambao ni aliyekuwa Rais wa Malawi Joyce Banda, aliyekuwa Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, aliyekuwa rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim, rais kutoka Ethiopia Sahle-Work Zewde na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tania Samia Suluhu Hassan.

Pia amesema kwa takwimu hizo zinaonesha dadi Januari 2021 kidunia maspika wa bunge ni asilimia 20.9, Manaibu spika wanawake wanawake ni asilimia 28.3 na wabunge wanawake katika nchi zote walikuwa ni asilimia 25.5 ambapo ni ongezeko la asilimia 42.2 kutoka asilimia 11.3 mwaka 1995.

Amesema Takwimu za utafiti uliofanywa na TGNP wa kuangalia ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi kwenye mihimilimitatu na vyama vya siasa unaonesha kuwepo kwa matumaini hasa kutokana na nia ya dhati ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Sulihi Haasan kutaka kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi.

Ni matarajio yangu kuwa warsa hii itajenga viongozi wanawake imara watakao enda kupunguza pengo la kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi sio tu vyuoni bali hadi kwenye nafasi nilizotaja bali kwenye nafasi zenye kufanya maamuzi yatakayosaidia wanawake pamoja na makundi yaliyopembezoni na jamii kunufaika na rasilimali za taifa.

Amesema wanacho waliofoka kwenye warsha hiyo wapo kwa niaba ya wanawake na jamii kubwa waliyoiacha katika maeneo yao hivyo ni muhimu kuyatendea haki yale yote watakaoyojifunza ili kuyafanyia kazi wa kushirikisha wananchi ili kuweza kuwainua na kufikia mabadiliko chanya wanayoyatamani.
Mkuu wa idara ya Maarifa, Utafiti na Uchambuzi Catherine Kasimbazi akisoma hotuba wakati wa kufungua warsha kwa wanafunzi  wa kike wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma. Bi Catherine alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
Baadhi ya wanafunzi  wa kike wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa idara ya Maarifa, Utafiti na Uchambuzi Catherine Kasimbazi  alipomwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi kwenye ufunguzi wa semina inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Makini  na Mwezeshaji wa semina hiyo Janeth John akitoa mada mbalimbali zinazohusu Uongozi kwa mtoto wa kike wakati wa kutoa mafunzo wa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
Baadhi ya wanafunzi  wa kike wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma wakichangia mada kwenye warsha iliyoandaliwa na  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) inayohusu Wanawake kushiriki kwenye Uongozi inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
Mwezeshaji wa warsha hiyo, Mary Nsemwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kuwanoa wanafunzi wa Kike waliopo vyuoni ili kushiriki kwenye Uongozi wanapokuwa vyuoni na kwenye jamii kwa ujumla warsha iliyoandaliwa na  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.
Mwananfunzi wa Mwaka wa Tatu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Zawadi Malombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nafasi za uongozi wa Watu wenye ulemavu warsha ya mafunzo ya wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu wapato 97 kutoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 katika ukumbi wa TGNP Mabibo.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad