HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2022

TGNP YATOA MAFUNZO KUHUSU CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA UPANGAJI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA

 


Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akitoa mafunzo kuhusu changamoto zinazokwamisha  na namna ya kukabiliana na changamoto kwenye upangaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia kwa Madiwani,  maafisa Mipango na Bajeti, Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa madawati ya Jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Mchumi kutoka Manispaa ya Kinondoni Mwantumu Magumbo akitolea ufafanuzi kuhusu mapendekezo ya kukabiliana na changamoto zinazokwamisha upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ikiwemo manispaa hiyo kubuni vyanzo zaidi vya mapato ili kuweza kupata pesa kwa ajili ya masuala ya masuala ya maendeleo ya kijamii, ushirikishwaji wa wadau ili kufanya uchechemuzi wa masula ya Kijinsia kwenye Manispaa hiyo pamoja na Serikali kuweka msisitizo kwenye masuala ya jinsia kama ilivyo kwenye masuala mengine ya Kitaifa wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango na Uratibu kutoka Halmashauri ya Kasulu Adili Mlowe akielezea changamoto wanazopitia kwenye wilaya hiyo kuhusu upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia ikiwemo ukosefu wa elumu kuhusu masuala yenye mrengo wa Kijinsia, Utashi wa kisiasa kwani kila mwanasiasa anakuwa na viupaumbele vyake vinavyopekelea kutozingatia upangaji na utekelezaji wa Bajeti yenye mlengo wa kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya Morogoro Vijijini Hamisi Mwambe changamoto zinazokwamisha upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia kama vile uelewa mdogo kuhusu upangaji wa Bajeti yenye mrengo wa kijinsia, Idara ya maendeleo ya jamii kutokupewa kiupaumbele katika upangaji wa bajeti pamoja na idara zoe mtambuka kutotenga bajeti yenye mrengo wa kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo kutoka Jiji la Dar es Salaam Judith Kihampa akiwasilisha changamoto zinazokwamisha na mapendekezo ya kukabiliana na Changamoto kwenye upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia ambapo changamoto alizoziwasilisha kwenye Jiji hilo ni  kukosa mwongozo maalum unaoelekeza kuhusu upangaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia, ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika kuibua viupaumbele vya pamoja na Ufinyu wa Bajeti kwenye Idara ya Maendeleo ya Jamii inayopelekea kutokutekeleza baadhi ya Shughuli  za kijamii ikiwemo mafunzo kwa jamii ili kutambua Bajeti yenye mrengo wa kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya  Muheza Erick Nehemiah akitolea ufafanuzi kuhusu changamoto zinazokwamisha upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia ikiwa ni ufinyu wa bajeti unaotokana na mapato hafifu ya Halmshauri hiyo, Uhaba wa watumishi pamoja na kuwa na viupambele vingi vinavyopelekea kushindwa kutekeleza bajeti kwa kuzingatia mrengo wa kijinsia  wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya Mbeya Vijijini Wazidi Mahenge akieleza kuhusu mapendekezo ya kukabiliana na changamoto za zinazokwamisha upangaji na utekelezaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na viongozi kupewa elimu juu y umuhimu wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia, usawa wa kijinisia kwenye uandaaji wa kamati zinazofanya maanuzi  pamoja na idara za maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii kuongezewa bajeti ili kuweza kufanya kazi yenye ufanisi wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Same Elisha Kapama akiwasilisha mapendekezo ya kukabiliana na changamoto za zinazokwamisha upangaji na utekelezaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia ikiwemo ushirikishwaji wa kutekeleza miradi yenye mrengo wa kijnsia, utoaji wa elimu zaidi yenye mrengo wa kijinsia pamoja na kuendelea kufanya ushawishi kwa serikali kuleta fedha kwa ajili ya miradi yenye mrengo wa kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Kishapu Ibrahim Sakulia akiwasilisha mada kuhusu changamoto zinazokwamisha upangaji na Utekelezaji kama vile ufinyu wa Bajeti, Baadhi ya jamii kutojua masuala ya kijinsia pamoja na kutotweka kiupaumbele kuhusu masuala ya kijinsia wakati wa upangaji wa bajeti wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakichangia mada kuhusu changamoto zinazokwamisha upangaji na Utekelezaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad