ROSE MUHANDO ATHIBITISHA KUNOGESHA TAMASHA LA KUMUOMBEA RAIS SAMIA JIJINI MWANZA, - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 2, 2022

ROSE MUHANDO ATHIBITISHA KUNOGESHA TAMASHA LA KUMUOMBEA RAIS SAMIA JIJINI MWANZA,

 
Maandalizi ya Tamasha la kumuombea Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na taifa kwa ujumla linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika .

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Novemba 2,2022 jijini Dar es Salaam,mratibu wa Tamasha hilo Kutoka Kampuni ya Msama Promotion Emmanuel Mabisa amesema maandalizi ya tamashaa hilo kubwa mpaka sasa yamekamilika.

"Mpaka dakika hii kila kitu kimekalika,yamebaki mambo madogo madogo ambayo kwa namna ilivyo yataongeza ladha ya tamasha hilo la aina yake kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Majirani wa mkoa huo"amesema Mabisa

Amesema kufuatia kukamilika kwa mandalizi hayo siku ya tamasha Maaskofu na Wachungaji mbalimbali watafanya maombi ya kumuombea Mhe Rais na Taifa kwa ujumla ili aendelee kuongoza Taifa wa Misingi ya Amani,Upendo na Utulivu.

Mabisa amesema mbali ya Viongozi hao wa Dini pia kutakuwepo na Waimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka Mataifa mbalimbali Ikiwemo Kenya,Uganda Rwana na Tanzania

"Kwa hiyo niwaombe Wakazi wa jiji la Mwanza na maeneo jirani wajitokeze kwa wingi kwa pamoja kuungana na viongozi wa dini kumuombea Rais wetu mpendwa Mhe.Samia Suluhu Hassani,lakini pia tumeweka kiingilia kiasi kidogo ili kila mmoja aweze kumudu kushiriki,kiwango ni shilingi 2000/= Kwa wakubwa na Kwa watoto shilingi 100/= " alisema Mabisa.

Kwa upande wake Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili hapa nchini,Rose Muhando amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.


"Tunajua Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ni mchapakazi na amejitoa kwa ajili ya Kuwatumikia Watanzania, kwa hiyo Dhamira ya Tamasha hili ni Kufanya Maombezi kwa ajili ya Kumuomba Mungu aweze kumfanyia wepesi Rais wetu kwenye Utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku,Watanzania nanyi mjitokeze kwa wingi katika tamasha hilo la Kumuombea Rais wetu " amesema Rose.

Rose Muhando amesema yeye anathibitisha kushiriki Tamasha Hilo na kuongeza kuwa ataungana na Waimbaji wengine katika tamasha hilo la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan,katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza hapo Novemba 6,2022.

Katika Hatua nyingine Rose Muhando ametaja mikoa mingine ambayo Tamasha hilo litafanyika kuwa ni Dodoma, Dar es salaam, Mbeya pamoja na Arusha.


Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Rose Muhando akizungumza na Waandishi wa Habari leo,akithibitisha kushiriki tamasha hilo la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na nchi Kwa ujumla litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mratibu wa Tamasha la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na nchi Kwa ujumla litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Emmanuel Mabisa akuzungumza na waandishi wa habari leo Novemba 2,2023 jijini Dar es Salaam wakati akieleza maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 6,2023 jijini Mwanza.Pichani kulia ni Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhando

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad