Hivi karibuni Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kilitangaza majina nane (8) ya makada wake walioteuliwa
kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ngazi ya
Taifa.
Makada hao ni pamoja na msomi mbobezi katika masuala ya
kihasibu na kifedha nchini CPA. Dkt. Edmund Bernard MNDOLWA ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa sasa, wengine ni Fadhili Rajabu MAGANYA,
Bakari Nampenya KALEMBO, Said Mohamed MOHAMED (DIMWA), Mwanamanga Juma
MWADUGA, Ally Maulid OTHMAN, Ali Khamis MASUDI na Hassan Haji ZAHARA.
Kampeni
za uchaguzi ndani ya Jumuiya hiyo zimeshika kasi huku mpaka sasa hali
ikionekana kuwa shwari kwa maana ya hakuna viashiria vya rushwa zaidi ya
vita ya maneno toka kila pande kutambiana kushinda nafasi hiyo ambayo
Mwenyekiti aliyopo sasa anapewa nafasi kubwa ya kutetea nafasi yake kwa
sababu ya kuwazidi sifa, uzoefu na uwezo wa kiuongozi washindani wake.
Uongozi
uliopo sasa unatajwa kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika
kipindi chao cha miaka mitano ikiwemo kuirejesha hadhi na heshima ya
jumuiya hiyo kwa kuimarisha utawala bora hali iliyopelekea kuimarika kwa
usimamizi na uendeshaji wa shule za jumuiya hiyo kiasi cha kufanya
vizuri katika mitihani ya kitaifa.
Mengine ni kurejesha mali
zilizoporwa huko nyuma, kuondoa vitendo vya ufujaji na ubadhirifu wa
mali za Jumuiya hiyo hali iliyowawezesha kujenga na kukamilisha ofisi
zake za makao makuu Dodoma badala ya kuendelea kuishi ofisi za kupanga.
Tunatambua
kwamba ni haki ya kila mgombea kuomba uongozi lakini suala la kuchagua
na kuchaguliwa ni maamuzi ya wapigakura. Hivyo wanachama walio wengi wa
Jumuiya hiyo wamewaasa wajumbe wanaokwenda kupiga kura kutumia haki yao
hiyo kwa kuchagua kiongozi wa kuendelea kuifanya Jumuiya hiyo kuwa
imara, yenye hadhi na heshima.
Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya
hiyo utafanyika tarehe 24-25 Novemba, 2022. Huku CCM ikiwakumbusha
wagombea wote kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama
kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.
Saturday, November 19, 2022

MAFANIKIO YAMBEBA MNDOLWA, ATAJWA KUTETEA KITI CHAKE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment