Kampuni
ya Coca-Cola Kwanza kupitia kampeni yake ya Biriani Friday na Coka
ambayo ilianza rasmi mwaka jana na kuendelea mpaka sasa, ikiwa na lengo
kubwa la kuendeleza utamaduni wa Misosi na Coca-Cola, ambapo huwa
tunatembelea wadau wetu mbalimbali wanao jishughulisha na upikaji
biriani kila Ijumaa kwa kuwaunga mkono na kuhakikisha tunawapatia wateja
wao wote Coca-Cola ya baridi pale wapatapo Biriani kwenye migahawa yao,
na kuwawezesha migahawa na vitendea kazi kama T-shirts, Aprons na
mikeka ya kutumia Biriani inapoliwa. Kampeni Birian Friday na Coke mpaka
sasa imeshafikia migahawa zaidi ya 50,kwa mikoa ya Dar-es salaam,
Dodoma, Morogoro, Tanga, Mtwara, Zanzibar na Mbeya.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutangaza Tamasha hilo
la Birian Friday na Coke, Meneja Biashara na Masoko Coca-Cola Kwanza
Wahida Mbaraka alisema kuwa tamasha la Birian Festival na Coke awamu ya
pili itafanyika Dodoma mnamo tarehe 26 Novemba mwaka huu.
‘Kwenye
tamasha ili, tutawakutanisha kwa Pamoja wapishi wa Biriani wa mkoa huu
na wateja wao, tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kipekee kabisa na
utofauti mkubwa, sababu tutaweza kupata Ladha pia ya vyakula vya asili
vya Dodoma, Vionjo vingi vya kiasili ambavyo vinabeba utaifa wetu, na
vile vile kuangalia mechi za Kombe la Dunia’, Mbaraka alisema.
Mbaraka
aliongeza kuwa kutakuwa na Migahawa Zaidi ya 15, Michezo ya Watoto
wetu, tukiburudishwa na Bendi ya Bushoke na Dj mkali Dj D-ommy Pamoja na
burudani nyengine nyingi, na zawadi mbali mbali.
Kupitia
jukwaa hili napeda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania wote,
wapenzi na wadau wa biriani na Coca-Cola, Familia, Marafiki kuja
kujionea na kushiriki kwenye utamaduni huu, Tanzania nchi yetu, Dodoma
ndio makao makuu yetu, Biriani na Coca-Cola ndio chaguo letu na Mpira wa
Kombe la dunia ndio raha yetu.Tarehe ni 26/11/22 ( Jumamosi), Mahali ni
viwanja vya wajenzi Maili Mbili Dodoma,kuanzia saa nne asubuhi,
aliongeza Mbaraka.Meneja
biashara na Masoko Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka (kati kati)
akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki wakati akitangaza
Tamasha la Birian Friday na Coke awamu ya pili ambalo litafanyika Dodoma
mwishoni mwa mwezi huu. Lengo la tamasha la Birian Friday na Coke ni
kuwakutanisha pamoja wapishi wa birian kwa kuendeleza utamanduni wa
Msosi na Coca-Cola. Kulia ni Meneja wa Beni ya Bushoke Anileth Bushoke.
No comments:
Post a Comment