HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2022

Benki ya Standard Chartered yashirikiana na SheFound kuelimisha wanawake kuhusu usalama wa mitandaoni (cyber security)

 

 
Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na SheFound wamewakutanisha wanawake zaidi ya 40 ambao ni wafanyabiashara mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto na fursa katika nafasi ya usalama kwenye mitandao.

Wafanyabiashara hao wanawake wamekutanishwa Novemba 23,2022 jijin Dar es es salaam,ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende aliwakilishwa na Jerry Agyeman-Boateng.

Akitoa maoni yake kwa niaba ya Benki, Jerry Agyeman-Boateng ambaye ni Mkuu wa Biashara Wateja Wakubwa, wa Kati na Taasisi za Fedha amesema lengo lao ni kuendesha biashara na ustawi kupitia utofauti wao wa kipekee.

Aidha amesema katika enzi ya kisasa ya kidijitali, wahalifu wa mtandao wanazidi kulenga mashirika mengi. Shirika lolote linaweza kulengwa na wahalifu wa mtandao iwapo hawatadhibitiwa ipasavyo .Tuna jukumu la kutekeleza ili kuhakikisha tunafahamishwa vyema kuhusu mashambulizi ya mtandaoni yanayoweza kutokea ili tunapofanya biashara tuwe salama."

Hivyo amesema benki hiyo inaishukuru SheFound kwa kushirikiana nayo kwenye kuwajengea uelewa wanawake kuhusu masuala ya usalama kwenye mitandao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SheFound Vannesa Kisowile pamoja na mambo mengine ameeleza kwamba zaidi ya asilimia 60 ya mandhari ya MSME barani Afrika yanaundwa na wanawake wajasiriamali kwa kutumia teknolojia.

Amesema ni muhimu kuongeza ufahamu kuhusu mambo ya usalama wa mtandao ili kupunguza matukio ya wizi yanayofanyika mtandaoni."Hii itasababisha ukuaji na uendelevu wa biasharapamoja na maendeleo ya jumla ya kijamii na kiuchumi."

Pia kulikuwa na mjadala ulihusisha wadau wengine wakiwemo wabobezi kwenye mambo ya biashara na tehama ambao walishiriki kutoa elimu na kubadilishana ujuzi na maarifa na wafanyabiashara hao.

Akizungumzia dhamira ya Benki ya kusaidia wanaoanza biashara, Busara Raymond ambaye ni Meneja wa Bidhaa za Fedha katika Benki ya Standard Chartered amesema Benki imewezesha kusaidia uanzishaji wa biashara kupitia SC Ventures ambacho ni kitengo cha biashara kinachohusika kuchochea na kukuza uvumbuzi. Pia kuwekeza kwenye teknolojia ya kifedha na kuchunguza mifumo mbadala ya biashara. SC Ventures iko wazi kwa biashara zote zinazoanzishwa ambazo zina maoni ya kibiashara yanayofaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania, Dkt Nkundwe Mwasaga akizungumza kwenye moja ya kongamano lililoandaliwa na Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na taasisi ya SheFound ambapo liliwakutanisha wanawake zaidi ya 40 ambao ni wafanyabiashara mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto na fursa katika nafasi ya usalama kwenye mitandao.



Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania, Dkt Nkundwe Mwasaga (wa tatu kulia) akizungumza kwenye moja ya kongamano lililoandaliwa na Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na SheFound ambapo liliwakutanisha wanawake zaidi ya 40 ambao ni wafanyabiashara mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto na fursa katika nafasi ya usalama kwenye mitandao.
Mtaalamu wa masuala ya 'IT' na Mhamasishaji wa Jamii kuhusu masuala ya Kifedha kutoka Benki ya Standard Chartered Bupe Mwakabaga akieleza jambo kwenye kongamano hilo lililoandaliwa na Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na taasisi ya SheFound ambapo liliwakutanisha wanawake zaidi ya 40 ambao ni wafanyabiashara mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto na fursa katika nafasi ya usalama kwenye mitandao.Pichani kushoto ni MKurugenzi wa Kampuni ya ya Meriitech Esther Mwasaga


Baadhi ya washiriki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano hilo









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad