HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MKUTANO WA COP27 NCHINI MISRI

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokuwa wakishiki kwenye Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri, wakati alipotembelea Banda la Tanzania katika maonyesho ya mkutano huo. Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi nyingi duniani zilizohudhuria mkutano huo kwa udhamini wa Benki ya CRDB kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira. Mkutano huo ulijadili jitihada za namna ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo kuchapusha miradi ya kupunguza kaboni kwenye hewa. Mkutano huo ulianza Novemba 6 hadi 19, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan  akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazinngira, Suleiman Jaffo alipokuwa akizungumza, wakati alipotembelea Banda la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
Maafisa wa benki ya CRDB wakiwa kwenye banda lao wakati wa Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazinngira, Suleiman Jaffo (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa benki ya CRDB wakati alipotembelea kwenye banda lao katika Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akikawa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waliokuwa wakishiki kwenye Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad