HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 7, 2022

ZIMAMOTO PWANI:TANZANIA IKO SALAMA DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

 

Kamishna Msaidizi Ardhi Mkoa wa Pwani Hussein Sadiki Idd akimkabidhi Kamishna Msaidizi ,Msemaji wa Jeshi la Zimamoto Puyo Nzalayaimisi hati ya kiwanja Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Kutoka kushoto ni Kamishna Ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Hussein Sadiki Idd akiwa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitaifa (SACF) Puyo Nzalayaimisi wakiwa kwenye maonesho yanayoendelea Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mrakibu Kamanda Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Pwani Jeniffer Shirima akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kwenye mkutano uliofanyika kwenye Maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani.

Na Khadija Kalili, KIBAHA
WAWEKEZAJI wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kupitisha ramani za majengo yao katika Ofisi za Makamanda wa Zimamoto kwa kila Mkoa ili kupata ushauri utakaosaidia kulinda usalama zaidi pale panapotokea majanga ya moto na kuathiri uwekezaji wao kazi.

Yamesemwa hayo leo na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto Kitaifa Kamishna Msaidizi Muandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi (SACF) alisema hayo alipotembelea kwenye banda la Zimamoto katika maonesho ya Wiki ya Uwekezaji na Viwanda Mkoa wa Pwani ambayo yanaendelea katika Viwanda vya Stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Amesema lengo haswa la kushiriki kwenye maonyesho hayo ni kutoa elimu kwa umm huku akiwahakilishia wawekezabi kwamba Tanzania iko salama dhidi ya majanga ya moto huku akitoa rai ya kuwataka kupitisha ramani za majengo yao kabya kuwekeza.

Aidha katika hatua ingine Kaimu Kamishna Ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Hussein Sadiki Idd amekabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Zimamoto iliyopo katika eneo la Halmashauri ya Chalinze yenye ukubwa wa meta za mraba 317 ambapo watajenga ofisi zake.

"Natoa shukrani za dhati kwa Wizara ya ardhi kwa kutambua unyeti wetu kwa jamii na kutupatia hati ya kiwanj hivyo suala la ujenzi tutalifikisha katika ngazi ya juu ambako ndiko watakakotekeleza.

Mrakibu Kamanda Zimamoto Mkoa wa Pwani Jeniffer Shirima alisema kuwa Mkoa umekua ukitoa mafunzo katika Wilaya zake kwa jamii kuhusiana na kuchukua tahadhari za majanga ya moto ikiwa ni pamoja kusimamia ujenzi wa mpangilio katika sehemu za makazi ya watu na biashara kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad