HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 8, 2022

UCHAGUZI WATINGA 16 BORA YA MICHUANO YA SHIMIWI TANGA

 

Timu ya kamba ya Bunge wanaume Katika Mchezo mwingine Bunge nao wamejikatia tiketi ya kucheza 16 bora baada ya kuwavuta Wizara ya mambo ya nje kwa mivuto miwili.

Timu ya Kamba ya wanaume ya Uchaguzi ikivutana na Bungeo jioni ya leo na kufuzu hatua ya 16 bora.
Kikosi cha Tume ya taifa ya Uchaguzi kilichopo jijini Tanga kewa michuano ya SHIMIWI 2022.TIMU za Kamba za wanaume na wanawake za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zimefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga.

Uchaguzi wamejikatia tiketi hiyo bada ya kuchezo mechi mbili za mtoano kutafuta kufuzu hatua ya 16 bora kwa kucheza na Bunge na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa zote za kundi E baada ya awali kufungana kwa pointi sita kila moja.

Wakishuka katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga jioni ya leo Oktoba 8,2022, Uchaguzi iliwavuta Bunge kwa mara nyingine kwa mivuto miwili na kupata alama mbili kisha kucheza tena na timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na kutoka nao sare ya mvuto mmoja kwa mmoja.

Matokeo ya jumla ya kundi E ni Uchaguzi alama 9, Bunge alama 8 na Wizara ya Mambo ya Nje alama 7 hivyo timu za Uchaguzi na Bunge wamefuzu kucheza hatua ya pili ya mashindano ya SHIMIWI 2022.

Kwa matokeo hayo sasa Uchaguzi wanaume inayoongoza kundi E itakutana na Wizara ya Elimu wakati Uchaguzi wanawake kutoka Kundi F itakutana na Wizara ya Katiba na Sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad