TUONDOE MFUMO DUME UNAOPOKONYA HAKI YA ELIMU KWA MTOTO WA KIKE KWENYE JAMII-JUVENALIUS - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 12, 2022

TUONDOE MFUMO DUME UNAOPOKONYA HAKI YA ELIMU KWA MTOTO WA KIKE KWENYE JAMII-JUVENALIUS

 

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

WATOTO zaidi ya 6,000 katika Halmashauri 12 nchini wamefikiwa kupitia mradi wa ELIMU KWA MTOTO WA KIKE unaotekelezwa na Shirika la Room to Read pamoja na kupanua wigo wa elimu kwa jamii juu kuondokana na mfumo dume unaopokonya haki ya mtoto wa kike kwenye sekta ya elimu.


Aidha mradi huo, sasa umejikita katika mkoa wa Pwani, Morogoro na Dar es Salaam ,lengo likiwa kupunguza tamaduni dhaifu zinazomkandamiza msichana.


Akielezea utekelezaji wa mradi huo wakati wa kilele cha siku ya mtoto wa kike Duniani huku Shirika hilo likiwa muandaaji wa jukwaa lililoshirikisha wadau wa elimu kwa msichana Kibaha, Mkoani Pwani, mkurugenzi wa Room to Read Tanzania Juvenalius Kuruletera alisema ,ni wakati wa jamii kuthamini usawa kwenye utoaji elimu bila ubaguzi.


"Tumeshuhudia baadhi ya tamaduni zinazomweka kando mtoto wa kike katika masuala mbalimbali,unakuta mtoto wa kike ndio apike,yeye ndio hapelekwi shule,anakatishwa masomo kwa kupata mimba ama kuozeshwa akiwa na umri mdogo":;Juvenalius.


"Tamaduni sio kitu kibaya,Ila ukienda kinyume matokeo yake yanakuwa sio mazuri, Tukubali kwenda na tamaduni zetu tulizozikuta ila kwa wakati uliopo "alifafanua .


Juvenalius alieleza, mafanikio ya mradi tangu uanze mwaka 2012 ,ni makubwa kwani utoro kwa watoto wa kike asilimia ni 0,utoaji wa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi , mtoto wa kike anapata kipaombele, ufaulu kwa mtoto wa kike umeongezeka, mimba za utotoni zinapungua.

Hata hivyo alieleza, maono ya mtoto wa kike yanawezekana endapo tukiungana kwa pamoja kumshika mkono.

Mgeni rasmi katika jukwaa hilo ,Ofisa elimu mkoa wa Pwani ,Sara Mlaki alieleza wakati ni sasa wa kukataa kumkandamizaji kwa mtoto wa kike.


"Tunatambua mchango wenu tangu mlipoanza kutekeleza mradi huu mwaka 2015 katika mkoa wa Pwani, Bagamoyo, Chalinze na sasa Kibaha"katika utoaji wa elimu na usomaji maktaba,fedha na ujasiliamali kwa msichana,ili waweze kujinasua kwenye changamoto zinazowakabili'"


"Siku hii ya leo tunapoadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani,ni fursa kwetu kutafakari kwa kina juu ya haki za mtoto wa kike, ulinzi na utoaji wa elimu ya kumlinda juu ya ukandamizaji na ukatili dhidi Yao"alielezea Sara.


Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mshamu Munde alilishukuru Shirika hilo kwa kutekeleza mradi huo kwenye shule nane ,kati ya hizo nne za msingi na nne nyingine ni za Sekondari.


Munde alitaja shule zilizonufaika kuwa ni shule za Sekondari Mwambisi,Bundikani,Nyumbu na Pichandege,huku shule za msingi zikiwa ni Kongowe , Maendeleo,Lulanzi na Kibaha.


Nao watoto wa kike Kibaha,Spora Munisi,Samira Maneno walisema wanakabiliwa na changamoto ya ushawishi wakiwa wanakwenda shule kutokana na umbali pia kuonekana ni viumbe dhaifu kwenye masomo ya sayansi.


Munisi alieleza ,wanaweza kutimiza ndoto zao kwakuwa wanajitambua kupitia njia ya kauli mbiu ya Room to Read "wakati wangu ni sasa nielimishe nishirikishe"nipe elimu usinipe mume.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad