HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 7, 2022

TCAA YAWAHAMASISHA WANAFUNZI WA SEKONDARI JUU YA FUSRA ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA


Mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Bi. Thamarat Abeid akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkwakwani wakati wa semina iliyofanyika shuleni hapo.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imetekeleza mkakati wake wa kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta ya Anga kwa njia ya semina.

Semina hizo zimefanyika katika jiji la Tanga ambapo imezihusisha Shule za Sekondari za Mkwakwani, Galanos na Shule ya Ufundi Tanga ambapo zaidi ya wanafunzi 2000 wamenufaika na elimu hiyo.

Afisa Elimu halmashauri ya jiji la Tanga Bw.Lusajo Kamwela alieleza kufurahishwa na mkakati huu kwani licha ya kuwafumbua macho wanafunzi na walimu unaongeza chachu ya kujisomea kwa wanafunzi na hii ni faida kwa mwanafunzi, shule na mkoa na Taifa kwa ujumla.

"Ninaishukuru sana TCAA kwa kuja na mpango huu, nakiri huu ni mwanzo mzuri kwa maendeleo wa taaluma. Niombe huu usiwe mwisho, kwa hapa Tanga shule bado ni nyingi na zote tungependa zifikiwe na mkakati huu hivyo mtakapo pata nafasi karibuni tena Tanga tupo tayari kuwapokea" alisema Bw. Lusajo

Akizungumza wakati wa semina hiyo Mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Bi. Thamart Abeid amewasisitza wanafunzi kuweka mkazo katika masomo ya sayansi ili waweze kukidhi vigezo vya kujiunga na masomo ya usafiri wa anga.
Naye Mkuu wa Shule ya sekondari Mkwakwani Bw. Stanley Mjema amesema kama shule wamepata bahati ya kuwa sehemu ya mkakati ambao umekuja wakati sahihi na kuahidi kuwa mabalozi kwa shule nyingine ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

Mkakati huu ulihusisha utoaji wa elimu juu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) uwepo wake, majukumu yake na magawanyiko wake wa kimajukumu, uelewa na fursa za chuo cha CATC pamoja na kozi zinazotolewa sifa na gharama zake, pamoja na elimu ya jumla ya uelewa kuhusiana na usafiri wa anga ilitolewa kwa wanafunzi na kuwataka kuwa mabalozi kwa wanafunzi wengine wa mkoa huo waliokosa nafasi hiyo na pia walipewa fursa ya kuuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi kuhusu masuala mbali mbali na majukumu ya TCAA.
Kaimu Meneja wa TCAA kituo cha Tanga Bw. Yusuph Twaha akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos akizungumza wakati wa semina iliyofanyika shuleni hapo.
Mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Bi. Thamarat Abeid akizungumza na wanafunzi wa shule ya Galanos wakati wa semina iliyofanyika shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Galanos waliofika mbele kuuliza maswali wakati wa semina iliyofanyika shuleni hapo
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga wakisiliza maelekezo yanayotolewa na wataalamu kutoka TCAA
Afisa Habari na Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Ally Changwila akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga wakati wa semina iliyofanyika shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad