HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 15, 2022

SHININI ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI UWT SIMANJIRO

 


Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa CCM Tanzania UWT Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamemchagua Anna Shinini kuwa Mwenyekiti wa UWT wa Wilaya hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo amemtangaza Shinini kushinda nafasi hiyo kwa kura 137.

Makota amesema wapiga kura walikuwa 223 ila kura mbili zimeharibika na kura halali zilikuwa 130.

Amesema wagombea walikuwa wawili ambapo Agnes Brown amepata kura 84 na Shinini kura 137.

"Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Shinini kuwa Mwenyekiti wa UWT wa wilaya ya Simanjiro," amesema Makota.

Akizungumza baada ya kushinda nafasi hiyo Shinini amewashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.


"Uchaguzi umeshapita hivyo hivi sasa tujipange kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu ipasavyo," amesema Shinini.


Hata hivyo, Agnes amekubali matokeo hayo na kudai kuwa asiyekubali kushindwa siyo mshindani.


Awali, uchaguzi wa UWT wilaya ya Simanjiro ulifanyika Septemba 24 mwaka huu ambapo kwa nafasi hiyo ya Mwenyekiti ililazimika kurudiwa mara mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad