-Asisitiza ajenda ya maendeleo kwa wananchi ipo katika mikono salama, Watanzania waendelee kumuunga mkono
KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni mwana maendeleo thabiti na
mwana CCM kindakindaki ambaye amedhamiria kuleta maendeleo.
Shaka amesema kuwa Rais Samia ameonyesha kwa vitendo uthunutu wa hali ya juu kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.
Ameyasema
hayo leo Oktoba 16, 2022 alipokaribishwa kusalimia wananchi wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa mjini Kibondo
akiwa katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma.
"Niwahakikishie
wana Kigoma na niwahakikishie Watanzania, ajenda ya maendeleo kwa Rais
Samia Suluhu Hassan ipo katika mikono salama. Maendeleo na Samia Suluhu
Hassan ni kama kulwa na doto," amesema.
Amesema Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kipaumbele chake cha kwanza ni maendeleo na hilo
limedhihirishwa na mkataba ambao Rais Samia, wabunge na madiwani
walikabidhiwa katika uchaguzi wa 2020.
”Tathimini ya kazi
mnayoifanya ndio hii ambayo leo sisi kama Chama tumekuwa na wewe mguu
kwa mguu, kuona namna gani ambavyo mmetekeleza yale ambayo tumewaahidi
Watanzania. Ndugu Mwenyekiti kama ni duka sisi CCM ndio wamiliki wa duka
hili...ninayo furaha kumwambia ndugu Samia Suluhu Hassan biashara
mnaifanya vizuri sana kuwaletea maendeleo Watanzania
Kwa mujibu
wa Shaka, CCM na wananchi ni mashuhuda wa kazi kubwa inayofanyika kila
siku kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Leo hii wote
tumeshuhudia wewe, timu yako na sisi CCM tumeshuhudia utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ulivyofanyika kwa ufanisi mkubwa
ndani ya Mkoa huu wa Kigoma.
"Tumeshuhudia utekelezaji wa Ibara
ya 83 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tuliahidi kuimarisha huduma za afya
kwa kujenga majengo ya kisasa na kusimamia upatikanaji wa vifaa tiba,
mmefanya kwa ufanisi mkubwa. Tumeshuhudia utekelezaji wa Ibara ya 100
inayohusu kuimarisha na kuhakikisha kwamba usaambazaji na upatikanaji wa
maji safi na salama ndani ya Mkoa huu wa Kigoma," amesema.
"Mheshimiwa
Rais tukijumlisha yote kwa ufupi umetekeleza kwa vitendo Ibara ya 46 na
49 ya kuimarisha na kufungua uchumi wa Wana-Kigoma na mikoa ya jirani.
Mheshimiwa Rais Mwenyezi Mungu akutunze ili Watanzania waendelee
kunufaika.
AVIPONGEZA VYAMA VYA UPINZANI KUUNGANA NA RAIS SAMIA
Aidha, Shaka amewashukuru viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani walioshiriki mkutano huo ili kumuunga mkono Rais Samia.
"Tunawashukuru
kwa kuja kuona mambo mazuri, karibuni tuungane pamoja tuijenge nchi
yetu, nchi ni moja na taifa ni moja , Rais Samia ameanza vizuri
kutuunganisha Watanzania mbali na imani zetu na itikadi zetu lakini
Tanzania ni moja," amesema.

No comments:
Post a Comment