RAIS SAMIA AZINDUA MATOKEO YA MWANZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 31, 2022

RAIS SAMIA AZINDUA MATOKEO YA MWANZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022

 Na Janeth Raphael MichuziTv.

HTIMAYE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi na kutangaza kuwa Tanzania ina jumla ya watu Milioni sitini na moja laki saba na elfu arobaini na moja na mia ishirini (61,741120).

Rais Samia ametangaza idadi hiyo ya watu leo Katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa kati ya Idadi hiyo ya watu Tanzania Bara ni watu 59,851,357 na Zanzibar ni watu 1,889,773.

Amefafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya watu Wanawake ni Milion 31,688790 sawa na asilimia 51 na wanaume ni milioni 30,53130 sawa na asilimia 49

Mhe.Rais Samia Ameeleza kuwa idadi hiyo ni Ongezeko la watu zaidi ya milioni 19 ukilinganisha na sensa ya miaka kumi iliyopita yaani 2012 ambapo kipindi hicho idadi ilikuwa milioni 44,928923.

Pamoja na hayo Mhe.Rais Samia ametaja Mikoa iliyoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ni Mkoa wa kwanza ni Dar-es-salaam ina watu milioni 5,38,3728 na Mwanza ina watu milioni 3,69,987 hii ni kwa upande wa Tanzania Bara.

Na kwa upande wa Zanzibar Mkoa unaoongoza ni Mjini Magharibi yenye idadi ya watu zaidi ya laki nane

Rais Samia amewaagiza viongozi katika ngazi zote kutumia muongozo aliyouzindua leo kwa ajili ya kuzidi kuwaletea maendeleo watanzania.

"Ni wajibu wa kila mdau kuanzia sekta binafsi na sekta za umma kutumia muongozo huu kuwahudumia wananchi kwa sababu tayari tuna idadi ya watu tunaotakiwa kuwahudumia katika kila nyanja iwe ni huduma ya Afya,elimu na kwinginepo,"Amesema Mhe.Rais


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad