HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2022

RAIS SAMIA ATEUA WAKILI MKUU WA SEIKALI NA NAIBU WAKE

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kama ifuatavyo:

1) Amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

2) Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bi. Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ametuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Oktoba, 2022.
Zuhura Yunus



Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad